Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MWAMBA wa demokrasia umeondoka nchini Tanzania!Hiyo ndio kauli iliyotolewa na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe wakati akitoa taarifa za Chama chao kwa umma kuhusu kufariki dunia kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Kabla ya Zitto kutoa taarifa hizo,Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi ndiyo aliyetangaza rasmi taarifa za kufariki kwa Maalim Seif na kuwaomba Watanzania kuwa watulivu kipidi hiki kigumu.Pia ametangaza siku saba za maombolezo na bendera itapepea nusu mlingoti.

Hivyo , Zitto wakati anazungumza leo Februari 17,2021 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine ameeleza kufariki dunia kwa Maalim Seif ni pigo kubwa katika nchi yetu.
"Maalim Seif Sharif Hamad enzi za uhai wake fikra zake na nia yake ilikuwa ni kuona Tanzania yenye demokrasia na Zanzibar ambayo Wazanzibar wanaishi kwa maridhiano, mwamba wa demokrasia umeodoka.

"Taarifa za mipango ya mazishi tutazitoa kwa umma baada ya mashauriano ya karibu kati yetu kama Chama na Serikali kwasababu Maalim Seif alikuwa kiongozi wa Serikali, na shughuli za mazishi yake yanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

"Na sisi kama Chama tutatoa ushirikiano wote kwa Serikali ili kuhakikisha tunamsitiri mzee wetu kwa heshima inayostahili.Nachukua fursa hii kama Kiongozi wa Chama kuwaomba Wazanzibar, wanachama wa ACT Wazalendo na Watanzania kuwa na utulivu katika kipindi hiki cha mtihani mkubwa sana wa kuondokewa na mwamba wa demokrasia ya Tanzania na mtetezi.

"Tunatoa pole kwa ndugu, familia na watoto wa marehemu na tutakuwa nao bega kwa bega , tutahakikisha mzee wetu anapata stara inayostahili,"amesema Zitto.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...