Na Woinde Shizza, Michuzi Tv-ARUSHA
Wizara ya maji haitakuwa kero kwa wananchi kwani watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wanatatua changamoto zote za maji.
Hayo yameelezwa na Waziri wa maji Jumaa Aweso
wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya maji wa mkoa wa Arusha
ambapo alisema kuwa kazi ya kushughulikia matatizo ya maji haijawashinda
wanaweza kutekeleza na fahari yao itakuwa ni kuona wananchi wanapata
maji.
Alieleza kuwa
maendeleo ya sekta ya maji yanaanza na watumishi hivyo wakashirikiane
katika kutatua matatizo ya maji huku wakitekeleza majukumu yao kwa
ukamilifu ili kutimiza hadhma ya upatikanaj wa maji safi na salama kwa
wananchi.
Alisema
dhamira ya serikali ni kupatikana kwa huduma muhimu ya maji safi salama
ya yakutosheleza wananchi ambapo serikali imekusudia kutenga bajeti ya
utekelezaji wa miradi ya maji ikiwamo mradi mkubwa wa maji unaoendelea
kutekelezwa mkoani Arusha.
“Kazi
haijatushinda tutafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha maji
yanapatikana maeneo yote yaliyo katika Mpango na katika hili niwaambie
tu kuwa mhandisi yoyote ambaye anayefikiria kuwa yupo kwaajili ya
kukwamisha wizara ya maji ajue kuwa anajikwamisha mwenyewe,”Alisema
Aweso.
Alisema uhuni
unaofanywa na baadhi ya watendaji ili kuhujumu miradi hivyo
wakahakikishe wanafanya kazi inavyostahili ili kutekeleza adhima ya Rais
lakini pia ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuhakikisha wananchi
wote wamapata huduma ya maji.
Kwa
upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Kimanta aliwataka watumishi wa
secta ya maji kutekeleza wajibu wao kazini na sio kusubiri kusukumwa
kwani maji ni moja ya sekta ambayo inamgusa mtu moja kwa moja.
Aliwasihi
kuisaidia serikali kutekeleza majukumu yake kwa weledi wa hali ya juu
pamoja na kuwashirikisha viongozi wa serikali changamoto zinazowakabili.
Naye
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (AUWSA) Mhandisi
Justin Rujomba aliahidi kukabidhi mradi wa maji wa Moita ifikapo April 9
mwaka huu ambapo watatekeleza kwa wakati na kwa ubora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...