Na Farida Saidy, Morogoro.

Wananchi wa vijiji vya Kigugu na mbogo Komtonga Wilayani Mvomero Mkoani Morogororo Wanaojishughulisha na kilimo cha Mpunga katika Skimu ya Umwagiliaji ya Kigugu wameshindwa kuendelea na shughuli za uzalisha wa zao hilo mara baada ya kuelezwa kuwa eneo hilo lipo chini ya Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii Jinsi wazee na watoto,Kitengo Ustawi wa jamii.

Wakulima hao wametoa kilio chao hicho mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Uvuvi na maji wakati ilipotembelea katika miradi hiyo ili kukagua shughuli zinazoendelea ambapo wamekuta wakulima hao wamesimamisha shughuli za kilimo kutokana na mgogoro huo. 

Akijibu hoja hizo NAIBU waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe amewaagiza wakulima kuendelea na shughuli zao za uzalisha wa zao la Mpunga katika Skimu  hiyo ya Uwagiliaji ya Kigugu kwa kuwa wizara haina taarifa juu ya suala hilo .

“Hao waliokuja walikuta hapa kuna mradi wa wizara ya kilimo hivyo kungekuwa na inshu wangekuja kutuona sisi watu wa wizara ya Kilimo”.Alisema Mhe Bashi.Hata hivyo Naibu waziri Bashe ameitaka serikali ya halmashuari ya wilaya ya Mvomero kupima eneo hilo lenye hakari mia nane ili liweze kupewa kwa wananchi wa vijiji hivyo ili kuendelea na uzalishaji wa zao la Mpunga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dakta Catherine Ishengoma ameitaka wizara kilimo kuhakikisha inashirikiana haraka na wizara ya afya ili kumaliza sitofahamu hiyo ili wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalisha wa mpunga kwa ufanisi Zaidi.

Kamati hiyo imetembelea miradi ya Skimu ya umwagiliaji pamoja na maghala la kuhifadhia mazao ya Mpunga  katika Wilaya Mvomero na Kilosa,huku ikionyesha kulidhika na ujenzi wa miundombino ya maghala pamoja na Skimu za umwagiliaji zilizojengwa kwa ufadhili wa Bank ya dunia chini ya mradi wa kuongeza uwezo zao la mpunga nchini na kusimamiwa na wizara ya Kilimo.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...