Watu watatu wakazi wa Jijinj Dar e s alaam, ya kuongoza genge la uhalifu na kusafirisha wadudu aina ya vinyonga wenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni nane.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Kija Luzungana ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imewataja washtakiwa hao kuwa ni Erick Ayo, Alli Ringo na Azizi Ndago.
Imedaiwa, Desemba 22, 2020 katika maeneo tofauti ndani ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Pwani kwa washtakiwa kwa pamoja na kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu na kusafirisha vinyonga wenye thamani ya Sh 8,546,889 mali ya Serikali ya Tanzania bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama Pori.
Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi na imeahirishwa hadi hadi Februari 29, 2021 itakapotajwa na washtakiwa wamepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kupeleka wadhamini wawili wenye utambulisho waliotakiwa kusaini bondi ya Sh milioni 2 kila mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...