Raisa Said,Tanga.
Ile changamoto ya Wazazi kuwaficha watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Mkoani Tanga imepungua baada ya elimu kutolewa kwa jamii.
Akizungumza na Waandishi wa habari Katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu kilichopo Jijini Tanga (YDCP) Mtoa tiba kwa vitendo Emanuel Mnyone alisema wazazi wengi wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kuwapeleka watoto Katika kliniki ilipo kituoni hapo tofauti na zamani.
" Kwasasa Wazazi wengi wamekuwa na msukumo mkubwa wa kuwafikisha watoto kituoni kwetu kwaajili ya kliniki na kufanya mazoezi tofauti na ilivokuwa siku za nyuma" Alisema Mratibu huyo
Mtoa tiba huyo alitumia fursa hiyo kuwashauri wanawake walio katika umri wa kuzaa kutumia vyakula vyenye Madini ya folic acid ili kuepuka kuzaa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi.
Alisisitiza kuwa ulaji wa mboga za majani pamoja na matunda kwa wingi husaidia kuzalisha Madini hayo kwa wingi ambayo yanasaidia kuwa ni kinga kwa mwanamke huyo.
Anaendelea kusema kuwa kuwa iwapo Madini hayo yatakuwepo ya kutosha katika mwili wa mama mjamzito Kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 90%kuzaliwa kwa mtoto wenye Afya Bora.
Kuhusu wasichana ambao wapo kwenye umri wa kubeba mimba amewashauri vyakula hivyo alivyoainisha na dawa za folic acid kabla ya ujauzito na miezi mitatu ya ujauzito ili kusaidia kuzaa watoto wenye Afya Bora.
Amina Omary Mkazi wa Kasera Jijini Tanga alisema wazazi wengi wanapojifungua mtoto mwenye matatizo kama hayo ikiwemo ulemavu wa viungo wamekuwa wanawaficha wakiamoni kuwa ni mambo ya ushirikina lakini kwa sasa elimu inayotolewa na watalaam wa afya imewafanya waanza kuwafichua na kufuata mashart wanayopewa.
" Ushauri tunaopewa na wataalam wa afya kuhusu vyakula umetufanya tubadilike na kufuata mashariti ikiwemo kwenda kliniki bila kuogopa tofauti na siku za nyuma " Alisisistiza Mama huyo .
Hivi karibuni Mjumbe wa Chama cha Wazazi wenye watoto wenye vkichwa kikubwa na mgongo wazo , Mkoa wa Tanga, Oscar Changala alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya kupata takwimu ya watoto wenye vichwa vikubwa kutokana na wazazi wengi wengi kuwaficha watoto hao .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...