Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Mkutano Mkuu wa 43 wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) umefanyika leo March 12, 2021 mjini Rabat nchini Morocco ukiambatana na Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Shirikisho hilo ambapo raia wa Afrika Kusini, Dkt. Patrice Motsepe (59) amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho hilo.

Dkt. Motsepe anakuwa Rais wa Saba wa Shirikisho hilo katika historia ya Soka la Afrika, ataanza majukumu yake ya Urais kwa kipindi cha miaka minne ijayo baada ya kuchaguliwa bila kupingwa katika Uchaguzi huo.

Katika Uchaguzi huo Wagombea watatu wa nafasi hiyo walijitoa katika kinyang’anyiro hicho. Waliojitoa ni Augustin Senghor, Ahmed Yahya na Jacques Anouma, Mkutano huo sambamba na Uchaguzi ulihudhuliwa na Rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino.

Pia ulihudhuriwa na Wajumbe mbalimbali wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Wachezaji wa zamani wa Afrika kama Samuel Eto’o sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba ya Tanzania, Barbara Gonzalez.

Dkt. Patrice Motsepe ni Mfanyabiashara wa Afrika Kusini, Mfadhili na Mmiliki na Rais wa Klabu ya Mamelodi Sundowns (Masandawana) ya Afrika Kusini.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...