Kamishna wa ulinzi wa ndani na mambo ya ndani Kaduna State, Ndg. Samuel Aruwan.


Watu wenye silaha wamewateka wanafunzi wa shule inayofahamika kama kama Federal College of Forestry Mechanism huko katika eneo la Mando Kaduna State huko Nigeria.

Taarifa za BBC, zinaeleza shuhuda amesema nusu ya wanafunzi waliotekwa hakuna mwanafunzi wa kiume kati ya waliotekwa.

Hayo yamethibitishwa na Kamishna wa ulinzi wa ndani  na mambo ya ndani Ndg.  Samuel Aruwan, ambae ameeleza kwamba ni kweli na uchunguzi unaendelea.

Msemaji wa Polisi, ASP Mohammed Jalige alisema idadi kamili ya wanafunzi hao wa kike waliotekwa bado haijajulikana.

Amesema Polisi wanafanya kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Nigeria kuwafuatilia watekaji na kuhakikisha wanawaokoa wanafunzi hao.

Kamishna wa ulinzi wa ndani na mambo ya ndani, Ndg. Samuel Aruwan, alifanya mahojiano na channels za TV mbalimbali Nigeria, alipokuwa akitoa taarifa hizo.

Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa mbalimbali za kisiasa, uchumi, biashara, burudani, michezo kijamii n.k.

#MichuziTV

#ChaguaKupambana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...