Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KAMPUNI ya GSM Foam imetambulisha bidhaa zake mpya za Godoro Maisha, Mito na Comfota huku ikielezea faida mbalimbali za kutumia bidhaa hizo mpya ambazo wamezitambulisha kwa Watanzania.

Akizungumza leo Machi 9, 2021 jijini Dar es Salaam wakati wa kutambulisha bidhaa hizo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa GSM Fatma Abdallah amewaambia Watanzania GSM inajivunia bidhaa zake zenye ubora.

Amefafanua "Sote ni mashahidi kwamba GSM imekuwa ikitoa huduma zenye ubora wa hali ya juu katika bidhaa na huduma zetu zote.Bidhaa zinazotambulishwa leo hii ni tatu Godoro Maisha, mito na Duvet almaarufu kama Comota.

"Hivyo basi napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wateja wetu ili waweze kujipatia bidhaa za kipekee na zenye ubora wa hali ya juu,"amesema Fatma na kuongeza GSM Foam Company ltd inajivunia kuwa na bidhaa mbalimbali zenye kukidhi mahitaji na matakwa ya watumiaji wa bidhaa zetu hasa zaidi magodoro , mito na Comfota.

Ameongeza hivi sasa tumejitahidi kusogeza huduma zao kwa kupitia matawi yao a mawakala mbalimbali kwa lengo la kuwafikia kila sehemu ndani ya nchi yetu.

Kuhusu fursa za uwekezaji Fatma amesema Serikali ya awamu ya Tano ikiongozwa na Rais Dk.John Magufuli imejidhatiti kuhakikisha kuwa wawekezaji wote wanapata mazingira bora kabisa ya uwekezaji na hivyo amewahamasisha wawekezaji wengine wawekeze nyumbani."Fursa zipo nyingi ya nchi yetu."



Kwa upande wake Ofisa Biashara Mkuu wa GSM Allan Chonjo amesema kupitia mtandao wao wa usambazaji wa bidhaa za GSM uliopo nchi nzima kwa maana ya matawi yao, mawakala na wauzaji wadogo wadogo pamoja na maduka ya fenicha wanaweza kuwafikia wateja wengi zaidi nchi nzima.

"GSM Foam inaendelea kusajili mawakala wapya watakaoweza kusambaza bidhaa zake nchi nzima.Unachotakiwa ni kutupigia namba yetu ya huduma kwa wateja, biashara hii inahitaji mitaji mikubwa na ni bidhaa zenye mzunguko mkubwa na faida nzuri,"amefafanua.

Wakati wa hafla hiyo, walikuwepo wawakilishi wa timu ya Yanga pamoja na baadhi ya wachezaji wao ambao nao walikuwa na mengi ya kushukuru toka kampuni ya GSM Foam kwa uwekezaji mkubwa ulioweza kuifanikisha Yanga kuwa hapo ilipo na katika ligi kuu mwaka huu wana uhakika wa kuchukua ubingwa.

Kwa upande wake Ofisa Biashara Mkuu wa Dar Young African, Senzo Mazingisa wanashukuru GSM Foam kwa udhamini wao na ushirikiano wao mkubwa kuifanya timu yao ya wananchi kufikia hapo walipo kuidi walivyotarajia.

Aidha imefafanuliwa GSM Foam Ltd ni kiwanda cha kuzalisha magodoro nchini Tanzania chenye makao makuu yake eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.

Maofisa wa GSM wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GSM Foam Fatma Abdallah( wa nne kulia) wakijiandaa kukata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa bidhaa zao mpya za magodoro, mito na Fomfota.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GSM Foam Ltd Fatma Abdallah(aliyevaa hijabu)Ofisa Biashara Mkuu wa Dar Young African(wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine na wachezaji wa timu ya Yanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kukata utepe kuashiria utambulisho wa bidha zao mpya ambazo wamezizindua leo jijini Dar es Salaam ambazo ni magodoro, mito na Comota.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GSM Foam Fatma Abdallah akizungumzia ubora bidhaa zao ambapo amewahimiza watanzania kuzinunua kwani faida zake ni nyingi kwa gharama nafuu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya GSM Foam Fatma Abdallah akizungumzia ubora bidhaa zao ambapo amewahimiza watanzania kuzinunua kwani faida zake ni nyingi kwa gharama nafuu.

Injinia Hers Said akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Ofisa Biashara Mkuu GSM Group of Companies na katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa GSM Fatma Abdallah.
Maofisa wa GSM , wawakilishi wa wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na baadhi ya wateja wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutambulishwa rasmi kwa bidhaa mpya za GSM.

Athonio Nugazi akizungumza mbele ya viongozi wa timu ya Yanga, maofisa wa GSM, wateja wa kampuni ya GSM pamoja na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya za GSM.


Sehemu ya maofisa wa GSM , viongzozi wa Yanga pamoja na wawakilishi wawachezaji wa timu ya Yanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwa bidhaa mpya za GSM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...