Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia taarifa ya utekelezaji wa maagizo yake kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu aliyoyatoa wakati wa kuwaapisha katika viwanja vya Ikulu, yakiwasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar wakifuatilia mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyoyatoa wakati wa kuwaapisha Mawaziri na Makatibu Wakuu, ikiwasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali (hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 9-3-2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakati wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu, wakati wa kuwaapisha, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...