Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo ametoa wito kwa wanaume kujitokeza kwa wingi kwenye mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Mara kwa ajili ya kupatiwa huduma ya Tohara.

Jafo ametoa wito huo leo jijini Dodoma wakati alipokua akipokea magari matatu kutoka kwa Taasisi ya Intra Health kwa ajili ya kusaidia huduma ya Tohara kwa wanaume kwenye mikoa minne ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya utoaji huduma hiyo, Jafo amewataka wanaume na vijana wa kiume ambao bado hawajafanyia huduma hiyo kujitokeza kwa wingi ili kufanyiwa huduma hiyo ambayo inachangia pia kuepusha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine ya Zinaa.

Amesema wanaume waliofanyiwa Tohara wana asilimia 60 ya kuepuka kupata maambukizi ya Ukimwi na magonjwa ya zinaa huku akiwataka kutoenda kufanya tohara kwa kigezo cha kufanya ngono zembe tu kwa sababu wameambiwa tohara huepusha maambukizi kwa asilimia 60.

Waziri Jafo pia amewaagiza Waganga Wakuu wote wa Mikoa ambayo huduma hiyo itaanzia kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri utakaowasaidia wanaume wote ambao hawajafanyia tohara wanapata huduma hiyo bila shida yoyote.

" Katika hili niwatake waganga wakuu kuhakikisha magari haya ya kisasa kabisa yenye vifaa bora ndani yake yanalindwa na vifaa vinatuzwa, maelekezo yangu ni kwamba magari haya yakalindwe kwa gharama zote na mimi nitafuatilia utunzaji wake, hatutomvumilia RMO yeyote ambaye gari itafanyiwa uharibifu kwenye Mkoa wake.

Lakini kwa upande wa wanaume mjitokeze kwa wingi, uwekezaji wa huduma hii ni mkubwa tena ikiwezekana mfanye mashindano kabisa ya vijiji na mikoa ambayo huduma hii itatolewa," Amesema Jafo.

Amewaipongeza Taasisi ya Intra Health kwa kuendelea kushirikiana na serikali kwa kipindi cha miongo miwili kwenye sekta ya afya nchini huku pia wakitimiza miaka 10  kwenye huduma hii ya tohara.

" Magari haya yanatolewa na Intra Health lakini kwa ufadhili wa Ofisi ya Rais wa Marekani, hii ni kuonesha jinsi gani serikali ya awamu tano chini ya Dk John Magufuli imekua na ushirikiano mzuri na wenzetu wa Marekani pamoja na taasisi binafsi katika kuwatumikia watanzania," Amesema Waziri Jafo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Intra Health nchini, Dk Lucy Mfuru ameipongeza serikali chini ya Rais Dk Magufuli kwa namna ambavyo imefanya jitihada kubwa katika kutoa huduma bora za afya kwa watanzania.

Dk Lucy amesema taasisi hiyo mpaka sasa ishatoa huduma ya Tohara kwa wanaume Milioni mbili nchini tangu waanze kutoa huduma hiyo ambapo pia wamefanyia maboresho vituo 10 vya afya ambavyo vimekua vikitumika kutoa huduma hiyo.

" Magari haya yamenunuliwa kwa ufadhili wa Ofisi ya Rais wa Marekani ni ya kisasa na ya kwanza nchini na yana vifaa bora vyenye uwezo mkubwa, ndani ya gari hizi kuna chumba cha uchunguzi, chumba cha upasuaji mdogo pamoja na chumba kidogo cha utoaji elimu kwa njia ya video," Amesema Dk Lucy.

Nae Mkurugenzi wa Afya kutoka Tamisemi, Dk Ntuli Kapologwe amesema vifaa vyote vilivyopo kwenye magari hayo na vile vilivyopo kwenye vituo vya afya vimegharimu Sh Bilioni 68 na vitakua msaada kwa wanaume na vijana wa kiume katika kufanyiwa tohara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selamani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara hiyo na Maafisa wa Taasisi ya Intra Health baada ya kukabidhiwa magari matatu kwa ajili ya utoaji huduma ya Tohara kwa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akiangalia vifaa vilivyopo kwenye magari ya utoaji huduma ya tohara kwa njia tembezi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa magari matatu ambayo yatakua yakitoa huduma ya Tohara kwa wanaume kwenye Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara. Magari hayo yametolewa na Taasisi ya Intra Health kwa ufadhili wa Ofisi ya Rais wa Marekani.
 


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selamani Jafo akipatiwa maelezo ya mojawapo ya TV iliyopo nje ya gari la utoaji huduma ya Tohara ambayo itakua ikitumika kutoa elimu kwa njia ya video.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...