Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Mbuge wakitiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika sekta ya ya kilimo ambapo pamoja na mambo mengine suala la kutafutiwa masoko limo.Picha na Richard Mwaikenda.
  Mahindi ya njano

Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
WIZARA ya Kilimo, imelitafutia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), soko la mahindi ya njano tani milioni moja Misri.

Neema hiyo ya soko la mahindi ya njano, imetangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerald Kusaya katika hafla ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika sekta ya kilimo iliyofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya jeshi hilo, wilayani Chamwino, Dodoma.

Amesema moja ya mambo watakayoshirikiana na JKT ni kuwatafutia masoko ya mazao kabla ya hata kuanza kuzalisha ili kuwa na uhakika ya kuyauza, hivyo ameihimiza JKT kaunza haraka kulima zao hilo ili kukidhi soko hilo.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Kusaya akielezea kuhusu soko hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...