Daktari Baraza Beneza akimhudumia mmoja wa watu waliofika kuulizia dawa ya asili ya Mwalaka ambayo hutibu kwa haraka maradhi ya kupumua na kubanwa mbavu iliyopewa kibali na Wizara ya Afya. Hapo ni eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.
Daktari Baraka Beneza akizungumzia ubora wa dawa ya asili ya Mwalaka ambayo hutibu maradhi mbalimbali yakiwemo ya kushindwa kupumua na kubanwa mbavu eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.


* Asema dawa ya Mwalaka imethibitishwa na Wizara

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wanaokumbwa na maradhi ya kushindwa kupumua vizuri na kubanwa mbavu  wameshauriwa wasipate taharuki kwani kuna dawa makini ya asili inayotibu ugonjwa huo.

Akizungumza Mkoani Dar es Salaam leo, Daktari Baraka Beneza amesema dawa ya Mwalaka inayotengenezwa nakampuni ya  Altenative International  Medicine imepata kibali cha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto baada ya kuonekana kufikia viwango.

Amesema dawa hiyo inapatikana kirahisi na kuna ushuhuda wa watu wengi ambao wameshaitumia na kupata matokeo chanya baada ya kupata matatzo ya kupumua, kukohoa  na kubanwa mbavu.

“Hii dawa inapatikana kirahisi Magomeni jengo la Butiama ilipo benki ya DTB, ni kinga na tiba hivyo nawashauri watu wakiona dalili za kubanwa mbavu na kushindwa kupumua vizuri watumie dawa hii muda mfupi sana watakuwa wameshapata suluhisho,” amesema.

Amesema  dawa hiyo inatengenezwa kitaalamu na Alternative International Medicine kwa kushirikiana na kampuni ya MICO  imewasaidia watu wengi waliokumbwa na shida ya kupumua, kukohoa na kubanwa mbavu.

“Watu wasitaharuki tena wanapopata matatizo ya aina hii badala yake waje wapate dozi hii ambayo ndani ya masaa machache itakuwa imemaliza changamoto inayowakabili,” amesema.

Abdallah Chondoma ambaye amewahi kuugua maradhi ya kushindwa kupumua, kubanwa mbavu na kukohoa sana alitoa ushuhuda kuwa baada ya kunywa dawa hiyo ya Mwalaka hivi sasa maisha yake yanaendelea kama kawaida.

Amesema alipata ugonjwa huo wakati akisafiri na basi kwenda msibani na wenzake lakini alipopatiwa dozi ya Mwalaka hali yake imetengemaa na anaendelea na kazi zake.

“Iliponishika nilikuwa nabanwa na mbavu, napumua kwa shida sana lakini dawa hii imenisaidia sana kwasababu ndani ya muda mfupi sana kifua changu kilifunguka na nikawa napumua vizuri na maumivu yaliisha,” amesema.

Amesema watanzania wanapaswa kuchangamkia dawa hiyo kwani imewasaidia wananchi wengi waliokuwa na changamoto ya kupumua ambao wametoa ushuhuda wa walivonufaika.

 “Dawa hii imesajiliwa rasmi na Wizara husika kwa namba TZ  17TM 0035 kwa hiyo serikali inatambua kwamba ni dawa nzuri inayotibu kwa uhakika na tulishaambiwa tuthamini vya ndani tusiamini kwamba kila kizuri lazima kitoke nje, watu watumie hii wajionee” amesema

Joyce Mwamtanga ambaye ni mjasiriamali wa vipuri Kariakoo amesema wiki tatu zilizopita alibanwa mbavu na kushindwa kupumua lakini alipotumia dawa ya Mwalaka alipata nafuu ndani ya muda mfupi.

“Kwa kweli tuthamini bidhaa zetu zinazozalishwa hapa nchini kwasababu hii dawa ya miti ya asili imenisaidia sana inanguvu kwasababu baada ya kuitumia haikupita nusu saa nikajiona wa kawaida kabisa,” amesema Joyce.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunaomba mfungue tawi kwa upande wa Zanzibar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...