Charles James, Michuzi TV
RAIS wa Msumbiji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika, Phelipe Nyusi amesema Tanzania na Afrika imepoteza kiongozi na mzalendo wa kweliAaa.
Rais Nyusi amesema kama ilivyokua kuamini kumuaga Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere ndivyo ilivyo ngumu leo kumuaga aliyekua Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.
Amesema kuaminika kwa Dk John Magufuli na watanzania kwenye Uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020 ni uthibitisho wake kwa watanzania kutokana na uwezo wake wa uongozi, weledi na uaminifu wake uliojaa uzalendo katika kuwatumikia watanzania.
" Tunawezaje kumuaga Dk Magufuli leo, tunawezaje kumuaga binadamu huyu mtoto wa kitanzania ambaye aliyatoa maisha yake katika kuwatumikia watanzania kwa uzalendo huku akifanya mambo makubwa kwenye Taifa hili.
Kama ilivyokua ngumu kumuaga Mwalimu Nyerere miaka 22 iliyopita ndivyo ilivyo ngumu leo kusimama hapa kumuaga Dk Magufuli, kiongozi aliyejawa maono ya kuwatumikia watanzania na aliyeupenda uafrika wake," Amesema Rais Nyusi.
Home
HABARI
TAARIFA
KAMA ILIVYOKUA NGUMU KUMUAGA NYERERE NDIVYO ILIVYO NGUMU KUMUAGA DK MAGUFULI- RAIS NYUSI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...