Charles James, Michuzi TV
TUMEMPOTEZA Rafiki! Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki imempoteza mwanamageuzi wa kweli na rafiki ambaye aliziunganisha Nchi zote zinazounda Jumuiya hiyo.
Akizungumza katika uwanja wa Jamhuri zinapofanyika shughuli za kumuaga aliyekua Rais wa Tanzania, Hayati Dk John Magufuli, Rais Kenyatta ametoa pole kwa Rais Samia Suluhu Hassan na watanzania kwa ujumla kufuatia kifo cha Dk Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.
Rais Kenyatta amesema kwenye uongozi wa Dk Magufuli aliwafundisha wana-jumuiya ya Afrika Mashariki kujitegemea kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuacha kutegemea misaada kutoka mataifa ya Nje.
" Afrika imempoteza mwanamageuzi wa kweli, mimi binafsi nimempoteza rafiki wa kweli ambaye tulipigana simu kila siku tukishirikiana katika mambo mbalimbali ya kujenga mataifa yetu.
Kwako Dada yangu Rais Samia Suluhu Hassan barabara umeoneshwa, sisi tupo nyuma yako nikuombe uendeleze kazi kubwa iliyoanzishwa na ndugu yetu Dk John Magufuli, niwaombe watanzania muungane mumpe ushirikiano Rais Samia ili aweze kuendeleza falsafa ya Dk Magufuli ya Hapa Kazi Tu, " Amesema Rais Kenyatta.
Amesifu jitihada kubwa zilizofanywa na Dk Magufuli katika kipindi chake cha uongozi kwa kujenga miundombinu ya barabara, nishati ya umeme, ujenzi wa kisasa huku akisema mchango wake katika ukuaji wa uchumi hautofutika kwa miaka yote.
Home
TAARIFA
RAIS KENYATTA: TUMEMPOTEZA RAFIKI AMBAYE ALITUFUNDISHA KUJITEGEMEA WENYEWE BILA MSAADA KUTOKA NJE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...