Na Jusline Marco-Manyara
Kamati ya bunge ya Nishati na Madini imeiagiza wizara ya madini nchini kuweka utaratibu mzuri wa ukaguzi katika geti la kuingia kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite yaliyopo Wilayani Simanjiro kwa kutoa kipaumbele kwenye haki za kila mmoja wakati wa upekuzi.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ziara ya kamati hiyo ambayo iliyofanyika Wilayani humo Mkoani Manyara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambayo iliidhinishiwa fedha katika bajeti iliyopita,Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Danstan Kitandula amesema wizara imechukuwa hatua ya kuongeza jengo la ukaguzi ili kurahisisha zoezi la kukagua watu wengi kwa wakati mmoja.
"Tayari tumesha fahamu aina ya kundi linalojihusisha na utoroshaji wa madini hivyo kwa kufahamu aina hiyo taratibu za upekuzi zitaimatishwa na katika ufanyaji wa upekuzi huo tutahakikisha hatutainhiza watu kwa makundi ambapo atakuwa anaingia mtu mmojammoja"alisisitiza Mhe.Kitandula
Aidha ametoa wito kwa wizara kuanza kuwasiliana na taasisi mbalimbali za teknolojia ili kuona ni mifumo gani ya kiteknolojia inaweza kutumika ambayo haitaleta madhara ya kiafya na wakati huohuo ikahakikisha usalama wa mali.
Ameeleza kuwa kama kamati wameridhishwa na ujenzi wa uzio huo jinsi ulivyosaidia kudhibiti rasilimali za nchi na kuongeza mapato kwa asilimia kubwa uoande wa madini ambapo pia kamati hiyo imeridhishwa na wizara jinsi ambavyo imekuwa sikivu kwa kutekeleza kila maagizo yaliyokuwa yakitolewa kwa wepesi kwa kufanya marekebisho.
Ameongeza kuwa kuanza kwa jitihada za kuanzishwa kwa soko la madini katika Mkoa wa Manyara kutarahisishia shughuli za uuzaji wa madini kufanyoka katika mkoa huo na kuwaondolea adha ya umbali kwa wachimbaji wa madini kuuza madini yao katika mkoa wa Arusha pia kutawavutia wawekezaji kuwekeza katika soko hilo kulingana na maagizo ya Mhe.Rais ilikuwa kila Mkoa uwe na soko la madini.
Kwa upande wake Wazirj aliyepewa dhamana katika wizara hiyo Mhe.Dotto Biteko amesema kuwa siyo nia ya serikali kufanya ukaguzi na upekuzi kwa namna ya kuwadhalilisha na kutweza utu wao bali nia ya serikali ni kuwafanya watu walindwe utu wao ambapo utaratibu uliopo sasa utaboreshwa na kufanya ukaguzi kwa mtu mmojammoja.
"Pamoja na kufanya maboresho hayo tutaweka utaratibu wa watu kuingia kufanya shughuli zao kwa zao kwa kuweka utaratibu wa watu kufanya kazi kwa shifti kwani mfumo wa dunia ulivyo sasa hivi siyo lazima watu wote wafanye kazi mchana wengine wanaweza kufanya kazi usiku hivyo tutafanya tathimi tuone kama watu wataweza kuwanya kazi kwa masaa 24 kwa shift ili tupunguze wingi wa watu kutoka jioni na wakati wa kuingia ."Alieleza Mhe.Biteko
Naye Mbunge wa Simanjiro Mhe.Ole Sendeka ameipongeza serikali kwa msimamo mpya waliokuja nao wa kuongezwa jengo la ukaguzi ambalo litagawanyika katika vyumba vidogovidogo tatizo la vyumba vya ukaguzi na kufanya kaguzi hizo kuthamini utu wa mtu hivyo kaguzi za hovyo za kukushanya watu wengi kwa wakati mmoja hazitafanyika tena.
Waziri wa Madini,Mhe.Doto Bitteko akitoa ufafanuzi juu changamoto ya ukaguzi na upekuzi kwa wafanyabiashara na wachimbaji wa madini wanaongia katika mgodi wa madini ya Tanzanite unaodhalilisha utu wao katika majumuisho ya ziara ya Kamati ya bunge ya nishati na madini iliyofanyika wilayani Simanjiro kwenye migodi ya madini ya Tanzanite Mererani Mkoani Manyara,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mhe.Ole Sendeka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...