Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Machi 10, 2021v imepokea taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayogharimu zaidi ya bilioni 10.3.

Akisoma taarifa ya utekelezaji ya Miradi hiyo mbele ya Kamati hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema Miradi hiyo inatekelezwa katika Taasisi za elimu zilizopo mkoani Arusha.

Amezitaja Taasisi hizo kuwa ni Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ambayo inatekeleza mradi wa ujenzi wa Maabara Changamano ambayo katika awamu ya kwanza umegharimu jumla ya Shilingi bilioni 2.3 wakati awamu ya pili mpaka sasa inagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 5.3.

Dk Akwilapo amesema Mradi mwingine wa zaidi ya Shilingi bilioni 5.7 unatekelezwa katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ni wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike ili
Kupunguza changamoto ya  wanafunzi kukaa  nje ya Chuo.  Ambapo kwa sasa 60% ya wanafunzi wanaishi nje ya chuo.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ni moja kati ya Taasisi  tatu zilizoanzishwa kwa lengo la kuinua na kuleta matokeo bora ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia na Uvumbuzi katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la shara ambapo Taasisi nyingine zipo Nigeria na Burkina Faso.

Katibu Mkuu huyo amesema Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kinatekeleza Mradi wa ukarabati na upanuzi ambapo ilitengewa kiasi cha Shilingi bilioni 1.5. Mradi huo unatekelezwa ili kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1978 na pia kukarabati majengo yaliyochakaa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ambapo amesema Kamati imeridhishwa na taarifa hiyo na hatua za utekelezaji zilizofikiwa.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Mikutano wa Bunge wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya wizara kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Katibu Mkuu Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwasilisha taarifa ya wizara kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Mikutano wa Bunge

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Staslaus Nyongo akisisitiza jambo wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu utekelezaji wa miradi ya Maendeleo

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Dkt. Leonard Akwilapo na Mhe. Hamis TaleTale wakiteta jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika viwanja vya Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...