Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu(wa pili kulia) akiwa ameshika zawadi ya picha ya nembo ya Taifa ambayo amekabidhiwa na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania(TWCC) wakati wa utoaji tuzo kwa wajasiriamali waliofanikiwa kuanzisha viwanda na biashara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa na TWCC.
Mkurugenzi wa Idara ya Mtoto katika Wizara hiyo Mwajuma Magwiza akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.John Jingu wakati wa tukio hilo.

Wanawake kutoka maeneo mbalimbali waliohudhuria tukio hilo la utoaji tuzo zilizotolewa na TWCC kwa mwaka 2021 wakiburudika kwa kucheza muziki uliokuwa ukipigwa wakati wa shughuli ikiendelea.

Mwenyekiti TWCC akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingra Ummy Mwalimu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingra Ummy Mwalimu ajadiliana jambo na viongozi wa TWCC.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu akiangalia moja ya jarida wakati wa hafla hiyo ikiendelea.
















Picha mbalimbali za matukio katika hafla ya utoaji wa tuzo katika maadhimisho ya wiki ya viwanda ya wanawake Tanzania kwa mwaka 2021. 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu amesema atahakikisha anaanzisha dirisha la wanawake katika Wizara  hiyo ili kuwezesha upatikanaji wa haraka wa vibali vya kimazingira kwa wanawake watakaokuwa wanahitaji kuanzisha viwanda na biashara mbalimbali vinavyohitaji vibali vya ofisi yake.

Aidha amesema umefika wakati kutambua adui ya mwanamke si mwanamke bali adui ya mwanamke ni umasikini, hivyo wanawake wote wana kila sababu ya kushikana mkono na kunyanyuana katika kuchangamkia fursa zilizopo nchini.

Waziri Ummy Mwalim ambaye aliyekuwa mgeni rasmi amesema hayo wakati akitoa hotuba yake kwenye hafla ya utoaji tuzo katika maadhimisho ya Wiki ya Viwanda ya Wanawake Tanzania kwa mwaka 2021 yaliyokwenda sambamba na utoaji tuzo za wanawake katika viwanda 2021.Tuzo hizo zimetolewa na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania(TWCC). 

Amefafanua katika kuhakikisha wanawake wanaendelea kupata fursa kuna mambo mengi Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli yakiwmo ya kuweka mazingira mazuri ya kufanya shughuli ambazo zitachangia kuleta uchumi nchini.

"Kuna hatua mbalimbali ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuweka mazingira mazuri ya wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo, nakumbuka nikiwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto nilikuwa mkereketwa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume, na hii nimekuwa nikiifanya kwa muda mrefu sana.

"Naomba kutumia fursa hii kuwahakikisha wanawake wote nchini katika Wizara ambayo niko sasa hivi, tutaanzisha dirisha ambalo lenyewe litakuwa mahususi kabisa kusaidia wanawake hasa katika kupata vibali vya kimazingira pindi wanapotaka kuanzisha viwanda au wanapohitaji aina yoyote ya kibali kutoka Wizara yetu.Tunataka wanawake wanapokuja kwetu wawe wanapewa kipaumbele kupita dirisha hilo,"amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha amewapongeza TWCC kwa kuandaa tuzo hizo kwa ajili ya kutambua mchango wa wanawake katika sekta ya viwanda na tuzo ambazo zimetolewa kwa taasisi za Serikali na binafsi zinakwenda kuchochea ukuaji wa maendeleo ya nchi yetu."Nchi yetu iko kwneye uchumi wa kati, na wanawake nao ni sehemu ya hatua hiyo ambayo nchi yetu imefikia."

Hata hivyo amesema umefika wakati wa kuhakikisha TWCC wanapewa jukumu la kuhakikisha wanawake ambao wanahitaji kuendelezwa kibiashara wanapita kwenye chemba hiyo ambayo ina uzoefu mkubwa katika eneo hilo badala ya kufikiria kaunzisha mashirikisho mengine mengi kwa ajili ya kusaidia wanawake.

Awali akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maedeleo ya Jamii) Mkurugenzi wa Idara ya Mtoto katika Wizara hiyo Mwajuma Magwiza amesema Serikali imeendelea kutenga fedha na kuwapatia wanawake fursa katika kushiriki shughul za kiuchumi na kupambana na umasikini  ili kujiletea maendeleo . 

Aidha Serikali imeweka mazingira rafiki kwa wanawake wajasiriamali kupata mikopo yenye masharti nafuu na kuondoa riba kwenye mikopo inayotokana na fedha hizo, hiyo ni pamoja na uanzishwaji mifuko 46 ya uwezeshaji kiuchumi ambayo yote inawezesha wanawake kiuchumi.

"Kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake kwa fedha zinazotengwa kupitia vyanzo vya ndani vya mamlaka za Serikali za Mitaa kiasi cha Sh. 63,489,080.00 zimetolewa kama mikopo na kunufaisha vikundi 938,802 kwa kipindi cha miaka mitano 2015 hadi 2020,"amesema.

Pia amesema katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba 2020jumla  ya Sh.bilioni nne zilitolewa kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.Serikali imefanya marekebisho ya sheria ya fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2018 ,kifungu cha 37 A, ambacho kinaelekeza mamlaka hizo kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani.

"Dirisha la Wanawake la Benki ya Posta Tanzania linaendeleza huduma zilizokuwa zikitolewa na iliyokuwa Benki ya Wanawake Tanzania kupitia dirisha hilo , kuanzia Julai 2020 hadi Desemba 2020, mikopo yenye thamani ya Sh.9,994,830,000 imetolewa kwa wajasiriamali 5,234 kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania Bara,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...