Kampuni ya uzalishaji wa Sukari ya Kilombero inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 584 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa kiwanda hicho Mkoani Morogoro ujenzi utakaoanza Mwezi Mei Mwaka huu pindi taratibu zitakapokamilika shughuli itakayochukua miaka miwili na miezi mitatu.
Kampuni hiyo ambayo imekuwa ni tija ya kiuchumi kwa
Wakulima wadogo wadogo kwa sasa ina wakulima elfu 66 wa zao la miwa
wanaofanya kazi na kiwanda cha uzalishaji wa Sukari ambao wanazalisha
tani 550,000 mpaka tani 600,000 kwa mwaka, kwa msimu mwaka 2018/2019
pekee walitoa tani za 629,000 na kulipwa kiasi cha shilingi bilioni 65
za kitanzania.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi wa Kituo
cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu Kazi amesema utekelezaji wa upanuzi
wa mradi huo ni swala ambalo ni la kushirikiana.
Mkurugenzi wa Kituo
cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu Kazi .


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...