Ni mtu wake wa karibu sana ambae anakwenda kutoa makala haya yanayohusu maisha binafsi ya Kanye West.
Mlinzi huyo aliwaambia waandishi wa habari, akisema kwamba vyombo vya habari vinasema, makala hii ni nzuri sana, ni ya saa 48 wakiipa jina la Lethal Weapon.
"Yote yatakayosika, yanatoka mdomoni mwangu, nilifanya kazi na Kanye West kama mlinzi wake kwà vipindi viwili tofauti" alisema Mlinzi huyo anayeitwa Stanulis.
Mlinzi huyo anajisifu kwamba, tukio moja ambalo halijulikani ni siku ya tukio la Saturday Night Live Breakdown, yeye alikaa siti ya mbele, siku hiyo wakati Kanye West akielekea chumbani alipigana .
Kila siku kulikuwa na kitu kipya , alieleza mlinzi huyo, akiiambia page six.
"Kuna stories nyingi zaidi za kueleza, sijawahi kuzisema popote" alisema.
Wakati alipofukuzwa kazi miaka mitano iliyopita alishawahi kusema kwamba, Kanye West alishawahi kupimwa na kukutwa na tatizo la kiakili (mental disorder).
Baada ya timu ya Kanye West kuona stori hii, wamemuona mtu ambae amepoteza muelekeo anatafuta kiki tu, na kutishia kumpeleka mahakamani, pia familia ya Kanye West pia imesema itakwenda mahakamani.
Stanulis mwenyewe anasema walishawahi kumtishia mara 2 kumshtaki, wakili wake aliingilia kesi hizo zikapotelea kusikojulikana.
Tusubiri tuone sakata hili litaishia wapi, makala itatoka? Na Kanye West atachukua hatua gani ni suala la kusubiria.
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa nzuri za kisiasa, burudani, michezo, kijamii n.k.
#MichuziTV
#ChaguaKupambana
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...