Hakimu wa Mahakama Kuu ya Lagos nchini Nigeria, S.S. Ogunsanya, jana Jumanne 09/03/2021, amemuhukumu kwenda gerezani, aliyekuwa meneja wa kampuni ya Dangote Industrial Limited, Ndg. Mojiso Aladejobi baada ya kufanya udanganyifu wa kujaribu kujipatia fedha kwà njia za udanganyifu kupitia bima, kiasi cha dola 32,000.
Meneja huyo amefungwa akiwa na wenzake wawili waliofahamika kwà majina ya Raymond Akanuli na Bqlogun Alaba.
Mashtaka hayo yaliletwa na Kitengo cha makosa ya Kiuchumi na Fedha, yakiwa ni makosa ya kula njaa na jaribio la kupata pesa kwà njia ya udanganyifu.
Mwaka 2014, Meneja huyo na wenzake walikula njama na kujaribu kujipatia fedha kwà njia za udanganyifu katika Kampuni hiyo.
Walifanya udanganyifu wa Bima ya ndege ya kampuni hiyo yenye usajili namba 5N-DGN ikiwa ni kinyume na kifungu namba 323 cha makosa ya jinai Lagos Nigeria sheria namba 11 ya mwaka 2011.
Endelea kufuatilia Ukurasa huu kwà taarifa, za kisiasa, uchumi, burudani, michezo,kijamii n.k.
#MichuziTV
#ChaguaKupambana
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...