Meneja Miradi ya Wanawake shirika la Actionaid, Amne Manangwa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika semina kuhusu Haki na uhusiano wa wafanyakazi mahala pa kazi ambayo ni Shera namba 6 ya mwaka 2004 sura namba 366 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Semina hiyo inaendelea kwenye hoteli ya Coral Beach Masaki Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam leo Jumamosi 13, 2021, Semina hiyo imeandaliwa na Shirika lilisilokuwa la Kiserikali la Actionaid.
Wakili wa kujitegemea, Aneny Nahum akiwasilisha mada kuhusu Haki na uhusiano wa wafanyakazi mahala pa kazi ambayo ni Shera namba 6 ya mwaka 2004 sura namba 366 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Semina hiyo inaendelea kwenye hoteli ya Coral Beach Masaki Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam leo Jumamosi 13, 2021, Semina hiyo imeandaliwa na Shirika lilisilokuwa la Kiserikali la Actionaid.

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la ActionAid limetoa mafuzo kwa waandishi wa habari vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini juu ya Mkataba wa Kimataifa wa shirika la kazi duniani ni naolenga kupinga Ukatili wa kijinsia mahali pa kazi.

Mkataba huo unaojulikana kama ILO Convention C-190 on Violence and Harrassment unavifungu vyote vinavyoweza kusaidia kupunguza, kuondoa unyanyasaji na ukatili mahala pakazi.

Akitoa maada wakati wa mafunzo hayo Wakili wa kujitegemea, Anneny Nahum alivitaja baadhi ya viashiria vya unyanyasaji na ukatili mahala pa kazi ni pamoja na Unynyasaji wa kimwili, Unyanyasaji kijinsia, Kiuchumi pamoja na kingono ambavyo mtu anaweza kufanyiwa na muajili, mfanyakazi au mwenzie.

Hata hivyo Nahum amesema kuwa vitendo vyote hivyo vinaweza kuondolewa ama kupunguzwa kama jamii kwa ujumla ikiwa na uelewa moja kwa moja kupitia serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kusaini makubaliano ya Mkataba huo ili uweze kutumika hapa nchini ingawa kunabaadhi ya vifungu vya sheria vipo katika katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

Amesema mchakato wa Kuridhia Mkataba wa C-190 utasaidia sana maendeleo ya nchi pamoja na Mfanyakazi mmoja mmoja hasa katika kipengele cha Uchumi kwani kila mtu ambaye ni mfanyakazi wa sekta binafsi na serikali kila mmoja atapata haki yake pasi na kunyanyaswa wala kufanyiwa ukatili wowote kwani katika mkataba huo unatafsiri ni nani mfanyakazi.

Kwa Upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali ya ActionAid, Anne Manangwa amesema kuwa lengo kubwa la mkataba huo ni Usalama na ulinzi Mahala pa kazi na kuona Tanzania yenye haki na Usawa.

"Sio Mwajili angalie nani wa kumpa ajira kuwa huyu ni Mremavu, mweusi, mweupe, mwanamke, Mwanaume, wotee wana haki ya kupata kazi huku kigezo kikubwa cha kupata ajira kiwe ni elimu ya mtu na uzoefu." Amesema Anne

Amesema kuwa Mifumo ya Sheria na sera za nchi zizingatie zaidi katika kujua mikataba mbalimbali ya kimataifa iliyoweza kusaidia Wanawake, watoto, watu wenye ulemavu kupata haki sawa na watu wengine katika jamii.

Licha ya hayo Mratibu wa Chama cha Wafanyakazi wa hifadhi, mahotelini, Majumbani na kazi nyinginezo Zanzibar (CHODAWU-Z), Fransica Clement amesema imeshakubali kujengwa kwa mahakama ya kuhukumu kesi za unyanyasaji wa kijinsia. Ambayo itakuwa na shughuli hiyo tuu kwani Nzanzibar matukio yanayoripotiwa ni macheche kuliko ambayo hayaripotiwi.

Amesema kuwa Mahakama hiyo itakapokuwa tayari wananchi kwa ujumla watakuwa na mahala pa kupeleka kesi zao za unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kiuchumi, Kimwili pamoja na Kisaikolojia ili wanaotenda makosa hayo waweze kuwajibishwa.

Fransisca ameiomba serikali kuridhia Mkataba huu wa Kimataifa wa shirika la kazi duniani wa C-190 uliotolewa kwaajili ya kuondoa ukatili wa kijinsia katika maeneo ya kazi, hata hivyo suala la ukatili wa kijinsia liwe la kitaifa ili jamiii kwa ujumla iweze kuondokana na Changamoto hii ili taifa la Tanzania liwe sawa mahala pa kazi.
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakati wa semina hiyo inayoendelea kwenye hoteli ya Coral Beachi manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam leo.
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakati wa semina hiyo inayoendelea kwenye hoteli ya Coral Beachi manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam leo.


Mratibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi,Mahoteli, Majumbani na Kazi Nyinginezo Zanzibar CHODAWU- Z, Fransisca Camilius Clement akiuliza swali wakati semina hiyo ikiendelea kulia ni Emmanuel Mabodo Afisa Mradi Shirika la Actionaid.
Afisa Mradi Shirika la Actionaid, Emmanuel Mabodo akifuatilia mada katika semina hiyo inayoendelea kwenye hoteli yaCoral Beach.
Waadnidh wa habari wakifatilia mada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...