Na Munir Shemweta, WANMM


Serikali imewaonya wamiliki wote wa ardhi wanaoharibu, kung'oa na kuhamisha alama za upimaji ardhi (Beacons) na kueleza kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kulipa faini ya shilingi 750, 000 au kifungo cha mwaka mmoja jela.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupitia kitengo chake cha Mawasiliano Serikalini ni kosa kisheria kufanya shughuli yoyote inayoweza kusababisha kuharibu, kung'oa au kuhamisha alama za upimaji.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebaini uwepo baadhi ya wananchi wanaoharibu, kung'oa na kuhamisha alama za upimaji na kubainisha kwamba, kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Kupitia taarifa yake Wizara ya Ardhi  imeeleza kuwa, kutokana na kukithiri vitendo hivyo inawakumbusha wananchi wote kuwa mtu yeyote atakayebainika kuharibu, kung'oa,  kuhamisha au kufanya shughuli  inayoweza kuharibu alama za upimaji ardhi atakuwa ametenda kosa la jinai na atawajibika kulipa faini shilingi 750,000 au kifungo cha mwaka mmoja jela au adhabu zote kwa pamoja.

Wizara ya Ardhi imewaasa wananchi wote kutojihusisha na vitendo hivyo kwa kuwa vinarudisha nyuma jitihada za serikali za kuongeza usalama wa miliki ardhi kwa wananchi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa ikipanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa lengo la kuongeza usalama wa miliki za ardhi kwa wananchi na maeneo yote yaliyopangwa na kupimwa yamewekewa alama za upimaji ardhini ( Beacons) kwa mujibu wa sheria ya upimaji ardhi sura ya 324.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...