Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero (mwenye suti nyeusi)akimkabidhi Leseni Mchungaji na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Christopher Ungani (katikati) na Kushuhudiwa na Mwanasheria wa Mwandamizi wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaolet Eseko katika hafla iliyofanyika Ofisi za Kanda hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Mchungaji Christopher Ungani akisaini taarifa mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa leseni na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA.)
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akisaini nyaraka za Leseni ya Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na masharti ya Leseni kwa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Mchungaji Christopher Ungani akitoa shukran mara baada ya kukabidhiwa leseni ya Televisheni.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero (mwenye suti) akiwa picha pamoja na viongozi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (walioshika Leseni ) na Mwanasheria Mwandamizi wa TCRA Vaolet Eseko.


*Mhandisi wa Kanda ya Mashariki TCRA ataka matakwa ya leseni kuzingatiwa 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi leseni ya   Kituo cha Televisheni cha  Hope  kilicho chini ya Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la  Waadventista  Wasabato Tanzania.

Akizungumza na kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba, Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa kituo hicho kifuate sheria na kanuni zilizopo katika leseni hiyo.

Amesema kuwa Mamlaka kama wadhibiti hawata acha kuchukua hatua pale panapotokea kukiukwa kwa leseni.Aidha amesema kuwa kupatikana kwa leseni ni jambo moja lakini jambo la kufuata nasharti ya leseni inavyotaka.

Amesema kuwa Mamlaka kama wadhibiti hawata acha kuchukua hatua pale panapotokea kukiukwa kwa leseni na kwamba kupatikana kwa leseni ni jambo moja lakini jambo la kufuata nasharti ya leseni inavyotaka ni muhimu zaidi .

Amesema kuwa Mamlaka kama wadhibiti hawata acha kuchukua hatua pale panapotokea kukiukwa kwa leseni.

Aidha amesema kuwa kupatikana kwa leseni ni jambo moja lakini jambo la kufuata nasharti ya leseni inavyotaka.

Kwa upande wake Mchungaji na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania Christopher Ungani amesema kuwa mpaka wanafika hatua ya kupokea leseni wamepata msaada mkubwa kutoka TCRA.

Amesema kuwa watafuata masharti ya leseni na kanuni pamoja na miongozo katika kutoa huduma ya kuhabarisha wananchi kitaifa.

Ungani amesema mara nyingine wakifika TCRA waende kwa mambo ya kujenga na sio ya ukiukaji wa leseni waliyopewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...