*GB moja kwa bei ya rejareja ilitakiwa kuuzwa sh.40000.
*GB1 ni sawa na Megabite (MB) 10,24
*Neema ya mawasiliano Chunya yabainishwa
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Mbeya
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Andrea amesema gharama za vifurushi 'Bando 'vya data ni rahisi kuliko kuliko kununua rejareja na Tanzania ndio nchi ambayo gharama za mawasiliano ziko chini ukilinganisha na nyingine ikiwemo Afrika Mashariki.
Vifurushi vya data vikiuzwa kwa njia ya rejareja ni watanzania wachache wangeweza kumudu gharama kwa data ,ujumbe mfupi.
Naibu Waziri ameyasema hayo wakati alipofanya ziara kuangalia upatikanaji wa mawasiliano kwa Mkoa wa Mbeya pamoja na Wilaya zake.
Amesema kwa bei ya rejareja ya data kwa megabite (MB) moja iko kati ya sh.9 hadi sh.40 hivyo kuwa na Gigabite moja (GB) ni sawa na sh.40,000.
Kundo amesema kutokana na ushindani na Sera wezeshi zilizozocheaa ushindani wa kampuni za simu kuja na vifurushi ambao ni ununuzi wa data kwa bei ya jumla.
Aidha amesema kuwa katika mazingira wezeshi sasa wanakuja na bei ya vifurushi kuwa chini zaidi ambapo Megabite moja itakuwa ni sh.2.03 ambapo itakuwa rahisi zaidi na kutoa mwanya wa mtu anapokaribia kumaliza vifurushi anaweza kuhamisha kwa watu wawili au kabla ya muda huo kuongeza vifurushi na kufanya kuongezeka vifurushi.
Naibu Waziri huyo amewataka watanzania kuendelea kutumia mawasiliano kwa ajili ya maendeleo kwani Wizara inaendelea kuboresha huduma kwa wananchi hao siku hadi siku.
Naibu Waziri Kundo alifafanunua kwa Gigabite Moja (GB1) ni sawa na Megabite (MB) 10,24.
"Nataka kuwa mkweli ya kuwa bei jumla ya Bando au vifurushi ni bei rahisi kuliko ununuzi wa rejareja na rejareja hiyo ingekuwepo basi maandamano yangetokea"
Katika ziara hiyo amepita katika Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuwa ameridhishwa huku Shirika la Posta (TPC) kudai kuwa ukarabati wa jengo katika Mkoa wa Mbeya kutumia zaidi ya milioni 48 haundeni na thamani ya fedha hiyo.
Amesema kuwa licha ya ukarabati huo kutoendana na thamani ya fedha isipokuwa wamejipanga katika kutoa huduma.
Mhandisi Kundo katika ziara hiyo ametembelea mradi wa Hallotel uliopo Kijiji cha Itumbi Kata ya Matundasi wilayani Chunya ambao fedha zake zimetolewa na serikali kupitia Mfuko Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) na kutaka kuongeza uwezo pamoja na mnara kuwa data ya 3G kwani fursa za biashara zipo.
Hata hivyo Mhandisi Kundo alimtaka Mtendaji wa Hallotel Mkoa wa Mbeya ampigie simu mkuu wake juu utekelezaji huo ambapo Naibu Waziri alijibibiwa hapohapo mbele ya wananchi wa kijiji cha Itumbi kuwa kufikia Mei 18 watakuwa wamekamilisha huku Jenereta wakasema wataweka ndani ya mwezi Machi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema kwa upande wa Mkoa wa Mbeya Mjini hakuna tatizo la mawasiliano changamoto ni baadhi ya maeneo ya wilaya lakini jitihada zake zimeanza kuchukuliwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka Mayeka amesema kuwa ujio wa Naibu Waziri umeleta neema kwa wanachunya kupata mawasiliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...