Charles James, Michuzi TV

Picha mbalimbali za wananchi waliojitokeza ndani ya uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma na wengine ambao walijipanga nje ya uwanja huo kwenye barabara za mitaa ya Dodoma kumuaga aliyekua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ambaye amefariki Dunia Machi 17 na kuagwa kitaifa jijini Dodoma Leo.

Wananchi hao waliojitokeza kwenye barabara za mitaa ya Dodoma ili kupata fursa ya kumuaga mpendwa wao kwani wengi wao walikosa nafasi ya kuingia uwanjani kutokana na uwanja kujaa idadi kubwa ya watu.

Mwili wa Hayati Dk Magufuli baada ya kuagwa ndani ya uwanja ulipitishwa katika barabara ya Bahi kuelekea Iringa Road kisha barabara ya Chuo Kikuu cha UDOM ambapo ulienda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Wananchi hao wamejitokeza wengi wakilia na wengine wakiwa na mabango ya kumuaga Dk Magufuli wakionesha upendo wao kwake kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya kwenye Jiji la Dodoma.

Ndani ya miaka mitano na miezi takribani mitatu ya uongozi wa Dk Magufuli Dodoma imepata mafanikio mengi ikiwemo kupata hadhi ya Jiji, Serikali kuhamia jijini hapa na kujengwa kwa Mji wa Kiserikali Mtumba, Soko la Kisasa la Job Ndugai, Stendi ya Kisasa ya Nanenane pamoja na Jiji hilo kuongoza kwa mtandao wa lami Tanzania.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...