Na Amiri Kilagalila,Njombe
WANANCHI wa kijiji cha Nundu kata ya Yakobi mkoani Njombe wamekataa taarifa ya mapato na matumizi iliyoandaliwa na mtendaji wa kijiji hicho kwa madai kwamba taarifa hiyo imeambatana na udanganyifu mwingi juu ya fedha zilizo changishwa kwa wananchi.
Hayo yamebainika katika mkutano wa wananchi na viongozi wa serikali ya kata ya Yakobi wa mapato na Matumizi ambapo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa matumizi ya fedha nyingi zilizo changishwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo wananchi wamegoma kufanyiwa hujuma dhidi ya fedha walizo changishwa.
“Utaratibu ni miezi mitatu mwananchi apate taarifa ya mapato na matumizi lakini kiongozi unapokuja unasema toka mwezi wa saba hatutakuelewa na taarifa ambayo imetolewa hapa hakuna haja ya kuwatafuta wataalamu,niombe taarifa hiyo ili mambo yaende taarifa hiyo ikaandaliwe upya”alisema Ally Mhagama (Dkt,Sagasaga) mkazi wa kijiji hicho.
Mwingine aliongeza kuwa “walipita nyumba kwa nyumba na kuchangisha naomba leo hii aseme kila kitongoji amechangisha shilingi ngapi na mimi nililipa elfu 40 tunataka kujua zilipatikanika shilingi ngapi” aliongeza mkazi wa Nundu
Ili kuwatendea haki wananchi wa kijiji cha Nundu, Afisa mtendaji wa kata Bi.Devotha Thomas Matias amelazimika kupokea matakwa ya wananchi na kumuagiza Mtendaji wa kijiji cha Nundu Jesca Mtove Pamoja na Viongozi wake kwenda kuandaa Taarifa Hiyo upya na Kuwasomea Wananchi.
“Taarifa ya mapato na matumizi tumeshaiacha kwasababu ina dosari na taarifa itasomwa vizuri katika mkutano unaofuata.”alisema Mtendaji
Kutokana na malalamiko ya wananchi diwani wa kata ya Yakobi Bw.Michael Uhaula ameungana na wananachi kuto ridhika na taarifa iliyo hivyo kuwataka viongozi kujipanga upya kuandaa taarifa hiyo kwa muda wa wiki mbili na kuwasomea wananchi huku akiwahamasisha wananchi kuacha tabia ya kususia shughuli za maendeleo.
“Habari ya michango hiyo taarifa hatujaipokea viongozi mkajipange ije hapa na tumeshakubaliana tarehe 23 tutakuwa na kikao hapa na ajenda ni moja tu baada ya hapo tuendelee na mambo mengine ya maendeleo.”alisema Uhaula
Aidha amewataka wananchi kuchangia michango wanayo kubaliana pamoja na kuwahamasisha wananchi kujishughulisha na kuacha tabia ya kulalamika kupanda vitu bei kama Mafuta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...