*************************************
Na Mwandishi wetu, Hanang’
Matukio Mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani Yaliyofanyika Kimkoa Katika Kata ya Basutu Wilayani Hanang.
Maadhimisho hayo yameongozwa na kauli mbiu isemayo..
*Wanawake katika Uongozi Chachu kufikia Dunia yenye Usawa*
Akihutubia katika Maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Hanang Ndugu *Ghaibu Lingo* kwa Niaba ya Mgeni Rasmi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara amewapongeza Wanawake Wote wa Mkoa wa Manyara kwa Jinsi ambavyo wameendelea kushika nafasi kubwa za maamuzi na hivo kuwepo kwa usawa miongoni mwa Jamii zetu kama ambavyo serikali yetu inatutaka.
“Hapa Hanang tunae Mwenyekiti wa Halmashauri ambae ni Mwanamke Mh Rose kamili, hivo hatuna shaka kwamba kwenye nafasi za uongozi tumeonyesha mfano mzuri na sasa ni  jukumu lenu kina mama mliopata nafasi hizo na wengine wote kuhakikisha mnazitumia vema kwa manufaa ya jamii zetu na Taifa kwa kwa Ujumla” alisema Ndugu Lingo.
Kupitia Maadhimisho hayo Wanawake wa Mkoa wa Manyara wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Mh Regina Ndege walitoa zawadi ya Shuka kwaajili ya Vitanda vya Wagonjwa katika kituo cha Afya Basutu.
 Semina mbalimbali za Ujasiriamali, Afya na Elimu ya Mazingira nazo hazikuachwa nyuma ambapo semina hizo zimelenga zaidi kuwavusha kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...