Na Amiri Kilagalila,Njombe
Zaidi ya watanzania 300 huathirika na tatizo la kifua kikuu (TB) kwa mwaka katika halmashauri ya mji wa Njombe huku Tanzania ni ikiwa ni zaidi ya watu 64,000 sawa na wagonjwa 176 kila siku kwa takwimu za mwaka 2011-2017
Amebainisha hayo Dkt,Kisulila Matanga mratibu wa kifua kikuu kutoka halmashauri ya mji wa Njombe kwa niaba ya mganga mkuu wa halmashauri wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari pamoja na kufuatilia mafunzo kwa wauzaji wa maduka muhimu ya binadamu yaliyofanyika mjini humo hii leo katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yaliyoanza Machi 16 na kuhitimishwa hii leo machi 24.
Aidha Dkt,Kisulila ametumia nafasi hiyo kumshukuru hayati Dkt,John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kwa ujenzi wa hospitali na vituo vya afya pamoja na kuongeza vifaa mbali vikiwemo vya kutambua tatizo hilo pamoja na kutibu ili kupunguza ongezeko la waathirika wa kifua kikuu nchini.
Amesema ugonjwa wa kifua kikuu umegawanyika katika madaraja mawili huku ugonjwa huo ukitibiwa bure nchini kutokana na juhudi mbali mbali zilizofanywa na serikali.
“Kuna madaraja mawili ya kifua kikuu moja ni kifua kikuu lakini pia na kifua kikuu sugu ambacho kinahitaji matibabu ambayo yako tofauti na matibabu ya kifua kikuu cha kawaida na wakati mwingine mgonjwa wa kifua kikuu anaingia mpaka ghalama lakini ikumbukwe matibabu ya kifua kikuu ni bure”alisema Kisulila
Vile vile ametaja dalili za maambukizi ya kifua kikuu (TB) yanayoambukizwa na vimelea aina ya bacteria wanaoathiri mfumo wa upumuaji huku ukiwa na dalili kamili tofauti na kifua (FLUE) ambacho huwa ni dalili ya ugonjwa Fulani “Mtu anapoona dalili kama kukohoa zaidi ya wiki mbili,homa za mara kwa mara,kutokwa na jasho jingi hasa usiku pamoja na kupungua uzito nashauri uende moja kwa moja kwenye kitengo cha kifua kikuu na ukoma utapokelewa na kupatiwa matibabu bure” alisema Kisulila
Hata hivyo ametaja makundi ya watu wanaoweza kupata maambukizi ya kifua kikuu likiwemo kundi la watu wanaokuwa kwenye eneo lenye giza kwa muda mrefu kama kuishi katika nyumba yenye madirisha madogo.
“Kwanza ni watu wanaokunywa pombe kwa wingi,wenye magonjwa ya muda mrefu ikiwemo saratani na sukari lakini kundi jingine ni la wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya HIV,wachimbaji wa madini na wale walio kwenye miingiliano mikubwa” Dkt,Kisulila Matanga alisema
Kwa upande wake Labani Mtega mratibu wa tiba asili na tiba mbadala halmashauri ya mji wa Njombe,licha ya kumshukuru hayati John Pombe Magufuli kwa kuweka sawa na kuwatengenezea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi kwa wataalamu wa tiba asili na tiba mabadala lakini pia amewashauri wagonjwa wa kifua kikuu kutumia lishe bora.
“Mgonjwa wa kifua kikuu sugu unashauriwa kutumia lishe bora ambayo nichakula chenye mchanganyiko wa aina moja kutoka kila kundi la vyakula mfano vya kujenga mwili,kuupa nguvu mwili,kulinda mwili,kuupa mwili joto ili kusaidia kuongeza kinga”alisema Laban Mtega
Naye Diana Simime mratibu wa huduma za upimaji HIV mjini Njombe amesema
“Tunamshukuru hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wetu wa awamu ya tano kwa ujenzi wa vituo vya afya katika nchi yetu na kuweka vifaa vya kutibu na kugundua magonjwa mabli mbali likiwemo hili la Kifua kikuu ambalo linatusumbua katika nchi yetu”
Dkt,Kisulila Matanga mratibu wa kifua kikuu kutoka halmashauri ya mji ya mji wa Njombe akifafanua namna ugonjwa wa kifua kikuu unavyoathiri watu wengi katika halmashauri ya mji wa Njombe huku akibainisha njia bora za kujikinga na tatizo hilo.Picha ya mtandaoni inayoonyesha kundi moja wapo hatarishi la watu ambao ni hatari zaidi kupata maambukizi ya kifua kikuu mara baada ya uvuataji wa sigara pampja na ulevi wa kupindukia.Picha ya mtandaoni inyoonyesha moja ya matibabu ikiwemo dozi pamoja na mgonjwa kifua kikuu ili kuonyesha ni jinsi gani ya kuweza kutibu maradhi hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...