*Mkurugenzi Mtendaji NIC Doriye awaasa wahitimu nidhamu katika kufikia mafanikio.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

 Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetoa kiasi cha shilingi Milioni 26 kwaajili ya ukarabati wa mabweni ya shule ya sekondari Jitegemee  ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na shule hiyo.

Fedha hizo zitatoka kufanya ukarabati baada ya kupata mchanganuo namna zitavyotumika kwani fedha hizo ni Zawatanzania.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dkt. Elirehema Doriye  katika Mahafali ya 27 ya kidato cha Sita shule ya Sekondari Jitegemee (JKT) yaliyofanyika katika Bwalo la shule hiyo  Jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji  wa NIC, Mhe.Dkt.Elirehema Doriye amesema menejimenti ya NIC imepokea wazo la menejimenti ya Shule ya Sekondari Jitegemee la kuwa na ushirikiano hususani katika uelimishaji umma na uwekazaji katika Bima.

Amesema kuwa kwa sasa Shirika lina mali zinazofikia sh.Trioni 100 tangu lilipoanzishwa.

"Ni kwa kweli niwaambie tu kuwa NIC kama mdau mkubwa wa maendeleo nchini kwa kuongozwa na sera ya kurudisha kwa jamii, mliomba kiasi cha shilingi Milioni Nane  tunachangia Shilingi Milioni 26 ambayo ni mara tatu ya mlioiomba". Amesema Dkt.Doriye.

Aidha Dkt. Doriye amewataka wahitimu kubadili maarifa yao kuwa ujuzi utakaowapa fursa za kutumia rasilimali zinazotuzunguka kuzalisha mali na kukuza biashara na pale mnapotoka mnaweza kujiajiri na Taifa likawa limepata mtaji wa vijana wenye uzalishaji.

 Amesema kuwa wale watakaoshindwa kuendelea na masomo moja kwa moja, wajishughulishe na shughuli rasmi za kuingiza mapato halali na kauli mbiuo ya kufikia mafanikio ni kuwekeza katika nidhamu.

"Msibweteke kuamini kuwa ajira ni zile za kuwa ofisini tu hapana, taifa linahitaji kila Mtanzania achape kazi popote alipo. Hii itasaidia katika kuongeza tija na pato kwa mtu mmoja mmoja na taifa hivyo huduma za kijamii kuimarika zaidi kutokana na uzalishaji unaofanyika" Amesema Dkt.Doriye.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Kanali Robert Kessy amesema wamekuwa wakijitahidi kuwaeleza wazazi na walezi wa wanafunzi kuhusu umuhimu wa ulipaji ada ingawa mpaka sasa umekuwa hafifu na kupelekea wanafunzi kurudishwa nyumbani ili kuweza kulipa ada hivyo kusababisha kukosa vipindi vya masomo darasani.

"Wazazi bado wanakuja kuomba uvumilivu kwasababu shule yetu ni yakusomesha watoto wote hasa maskini huwa tunawasikiliza ila mrejesho wenu wazazi na walezi sio mzuri". Amesema Kanali Kessy

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dkt.Elirehema Doriye akizungumza katika mahafali ya 27 ya Kidato Cha Sita Shule ya Sekondari Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Jitegemee yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule ya Sekondari JKT Jitegemee Brigedia Mstaafu Lawrence Magere akitoa taarifa kwa Mgeni Rasmi katika mahafali 27  ya Kidato cha Sita ya shule hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa shule ya Sekondari JKT Jitegemee Kanali Robert Kessy akitoa historia fupi kuhusiana na shule hiyo katika mahafali ya 27 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Mkuu wa Shule Utawala Meja Waryoba  akitoa utambulisho kwa Watendaji na Walimu wa Shule ya Sekondari JKT Jitegemee katika Mahafali ya 27 ya Kidato cha Sita yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) akiwakabidhi vyeti wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali kwenye mahafali ya 27 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari JKT Jitegemee yalifanyika katika viwanja vya shule hiyo Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu watarajiwa wa Shule ya Sekondari JKT Jitegemee  wakiingia na gwaride kwenye mahafali ya 27 ya shule hiyo yaliyofanyika  katika viwanja vya shule hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dkt.Elirehema Doriye mwenye sikafu akiongozana na Mkuu wa shule ya Sekondari JKT Jitegemee kwenye Mahafali ya 27 ya Shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...