*Basila aeleza sababu ya warembo wake kutopenda skendo
Na Khadija Seif, Michuzi tv
MUANDAAJI Wa Shindano la urembo la Miss Tanzania Basila Mwanukuzi ameiomba Serikali kuendeleza kukuza utalii kupitia sekta mbalimbali ikiwemo sekta hiyo ya urembo.
Akizungumza na Michuzi TV mara baada ya kufungua rasmi shindano la Miss Tanzania 2021 na kutoa semina kwa mawakala wa Miss Kanda na Miss
Wanaowakilisha Mikoani Basila amesema, Sekta hiyo ya urembo imekua ikionyesha jitihada za dhati kukuza utalii wa ndani.
"Awali warembo walikua wakitembelea vivutio vya utalii na kuvitangaza ili vitambulike na watu wahamasike kutembelea vivutio hivyo." Amesema.
Mwanukuzi amesema waliamabwende wanaopita Miss Tanzania wamekuwa wakitembelea vivutio vya utalii pamoja na kuwajengea utamaduni wa kuhakikisha warembo hawatoki kwenye mstari wa maadili ya Kitanzania ikiwemo lugha, mavazi, vyakula pamoja na kuwapa nafasi washiriki kutambulisha tamaduni zao.
Aidha Mwanukuzi amempongeza Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha nia ya kutoa ushirikiano katika sekta ya utalii.
Vilevile amewapongeza washindi wa shindano la Miss Tanzania waliovaa taji lilo tangu aanze kuendesha Shindano hilo na kuendelea kuijengea heshima Kampuni ya 'The look.'
"Sijapata taarifa yoyote wala skendo za Miss wangu ama washiriki waliowahi kushiriki Miss Tanzania kuwa wana maadili mabaya." Amesisitiza Mwanukuzi.
Kwa upande wake Wakala shindano hilo kutoka Dodoma Alexander Nikita amesema mashindano ya Miss Tanzania ni mojawapo ya fursa kwa watoto wa kike hasa Wasichana kuonyesha kwa vipaji vyao.
"Miss Tanzania ni moja ya jukwaa pana ambalo linatoa fursa mbalimbali ikiwemo kutambulika na kujitolea kwenye jamii kama wanavofanya washiriki na washindi wanaopatikana kwenye shindano hilo." Amesema.
Nikita amesema, wamejipanga vizuri kwa mwaka huu katika Mchakato wa kupatikana Miiss Dodoma.
"Watarajie Kupatikana kwa Washiriki ambao Wataingia kwenye michujo mbalimbali na hatimaye Kupatikana kwa Mwakilishi wa Miss Tanzania, hivyo tumejipangaa vizuri na tutaanza Mchakato hivi karibu na tutegemee kupata mrembo na mwenye akili ya kusaidia jamii na Dodoma tuna mfano mzuri happyness Watimanywa alituwakilisha vizuri." Amesema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...