Na Amiri Kilagalila,Njombe
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoani Njombe imefanikiwa
kuokoa kiasi cha shilingi milioni 29,802,646 kutoka kwa wadaiwa sugu
waliokopa katika vyama vya ushirika vya AMCOS, SACCOS pamoja na benki ya
Njocoba.
Hayo yamesemwa
leo na mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe Kassim Ephrem wakati alipokuwa
akitoa taarifa ya utekelezaji wa oparesheni ya taasisi hiyo kwa kipindi
cha miezi mitatu iliyofanyika hapa mkoani Njombe.
Amesema
katika vyama vya AMCOS na SACCOS shilingi milioni 23,003, 000
zimeokolewa kutoka kwa wadaiwa hao huku kiasi cha milioni 6,799,646
kikikusanywa kutoka wadaiwa wa benki ya Njocoba.
Amesema
taasisi hiyo pia imesaidia kukusanya jumla ya shilingi milioni
22,462,886.26 ambazo zimeokolewa kutoka kwa wadaiwa sugu wa mfuko wa
taifa wa hifadhi jamii (NSSF) tangu walipoanza zoezi la kuwafuatilia
waajiri ambao hawawasilishi michango ya wanachama wa mifuko hiyo.
Amesema
katika zoezi hilo Takukuru pia imefanikiwa kukusanya na kuokoa shilingi
milioni 31,635,000 kutoka kwa wadaiwa sugu wa mfuko wa pembejeo za
kilimo (AITF) ambao ni wadaiwa mmoja mmoja.
"Napenda
kutumia fursa hii kuwahimiza waajiri wote kuhakikisha kuwa
wanawasilisha kwa wakati makato ya michango ya watumishi wao kwa mifuko
ya hifadhi ya jamii bila shuruti" amesema Kassim.
Amesema
katika kuchunguza makosa ya rushwa kama sehemu ya majukumu ya taasisi
hiyo wameweza kuokoa kiasi cha shilingi milioni 67,931,432 ambazo kama
wasingeingilia kati zingeishia katika mikono ya wahalifu na kushindwa
kufanya kazi iliyokusudiwa.
Amesema
kuwa fedha hizo zimeokolewa kutokana na taarifa mbalimbali ambazo
walizipokea zikihusisha tuhuma za rushwa na ubadhilifu.
Amesema
pamoja na kuokoa fedha hizo taasisi hiyo imeendesha jumla ya kesi 10
katika mahakama za wilaya ya Njombe na Makete zilizotokana na makosa
mbalimbali yakiwemo ya rushwa na yasiyo ya rushwa.
Amesema
katika kipindi hicho kesi nne zilizokuwa zikiendeshwa katika mahakama
ya wilaya ya Makete zimetolewa hukumu na watuhumiwa katika kesi hizo
zote walitiwa hatiani.
"Washtakiwa
watatu walihukumiwa kila mmoja kifungo cha miaka mitatu jela na
kutakiwa kurejesha fedha walizofanyia ubadhilifu kwenye halmashauri ya
wilaya Makete pindi wamalizapo vifungo vyao" amesema Kassim.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...