Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wananchi
wa kijiji cha luduga kilichopo wilaya ya wanging'ombe mkoani Njombe
wamelalamikia kitendo cha viongozi wa kijiji hicho kuwakamata na
kuwaweka ndani ya ofisi kina mama wakiwa na watoto wadogo kwa tuhuma za
kutolipa mchango wa ujenzi wa shule ya sekondari.
Wakizungumza
na mwandishi wetu baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa licha ya kuwa na
matatizo ya kiafya na kuwa na watoto wadogo bado viongozi hao
wamewakamata na kuwafunga kwa zaidi ya saa 9.
Akizungumzia
kuhusiana na malalamiko hayo mwenyekiti wa kijiji hicho AMADY OMARY
MPANYE amekiri kuwepo kwa zoezi hilo la kuwakamata wale wote ambao
hawajalipa mchango na kueleza kuwa hajapokea changamoto ya wananchi hao
wanaodai wamefungwa wakiwa na watoto wadogo.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Luduga Hassan Ngella amesema kuwa hana
taarifa ya wananchi hao kufungwa wakiwa na watoto wadogo na wenye
matatizo ya kiafya na kuwataka kuendelea kutoa mchango wa ujenzi wa
shule ya sekondari ya luduga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...