MSHINDI Wa Tuzo ya Malkia wa Nguvu katika kipengele cha Afya na Ustawi wa Jamii Prof. Paulina Mella ambaye pia ni muasisi wa Shahada ya uuguzi nchini amewashauri wasichana kusomea fani ya uuguzi ili kuweza kuokoa maisha ya wanawake ya watanzania kuwa ujumla pamoja na kupata fadhila kutoka kwa Mungu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha siku ya Malkia wa Nguvu iliyobeba kauli mbiu ya "Malkia wa Nguvu, Ingia Ulingoni" na kuandaliwa na Clouds Media Group (CMG,) Prof. Mella amesema, fani ya uuguzi ni ya kujitolea katika kuokoa maisha ya wengine na amewashauri wasichana kujitoa na kusomea fani hiyo ambayo inatolewa katika vyuo vikuu vipatavyo saba nchini.

Amesema kuwa tangu astaafu bado anafundisha fani ya uuguzi aliyoitumikia kwa miaka mingi na kupitia changamoto nyingi katika kuyafikia malengo ya kuiletea thamani fani ya uuguzi na wauguzi katika jamii.

Aidha ameishukuru Clouds Media kwa kutambua mchango wake na kumpa heshima ya kumpa tuzo hiyo kwa kuthamini alichokifanya katika jamii na kuwashauri kuendeleza juhudi za kuwatambua Malkia wa Nguvu ili kuleta motisha kwa wanawake wengi zaidi katika jam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...