Kampuni ya
Asfa Hose Service and Maintenance Support Ltd imeshiriki Maonesho ya
Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yaliyoandaliwa na Taasisi ya GS1 Tanzania
iliyopo chini ya Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kahama mkoani
Shinyanga.
Akizungumza
leo Mei 26,2021 kwenye maonesho hayo yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi Nyihogo Kahama, Afisa Masoko wa Kampuni ya Asfa Hose Service
and Maintenance Support Ltd, Gabriel Mathew amesema wameshiriki maonesho hayo kwa ajili ya kutangaza Kampuni
yao.
“Tumekuja kutangaza Kampuni yetu ya Asfa Hose Service and Maintenance Support yenye makao makuu Mjini Kahama mkoani Shinyanga na matawi yake Tabora na Mwanza na kutoa elimu kuhusu huduma tunazotoa”,amesema.
Amesema
lengo jingine la kushiriki maonesho hayo ni Kuibua fursa mbalimbali
zinazojitokeza kwa wajasiriamali walioshiriki maonesho na kutanua wigo wa
mawasiliano (Connection) kwa wadau mbalimbali,kujifunza na kuongeza maarifa
kupitia washiriki wa maonesho.
Amefafanua
kuwa Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Ltd inajihusisha na
kubana hose pipe,kuuza vipuli vya mitambo,mashine na magari,kuuza vifaa vya
kujikinga na hatari kazini (PPE),kuuza Filters za aina zote,ufundi wa
kutengeneza mitambo mikubwa migodini, Pampu aina zote na magari.
“Hali
kadhalika tunajihusisha na kuchomelea na kuunganisha mitambo na kuagiza magari
mapya kutoka nje ya nchi, kukodisha mashine kama Crane, Fork lift, Excavator,
Dozer,Grader,Rolla”,ameeleza Mathew.
Ameongeza
kuwa Asfa Hose pia wanajihusisha na utoaji elimu kwa wachimbaji wadogo na jamii
kuhusu umuhimu wa kutumia vifaa vya kujikinga na hatari kazini (PPE), usalama
kazini na utunzaji mazingira pamoja na masuala
ya Burudani ikiwemo kuandaa Matamasha ya michezo na muziki.
Huduma
zinazotolewa kwenye Kampuni ya Asfa Hose Service and Maintenance Support Ltd ni
Line Boring, Civil Work, Machine Hire, Supply of PPE, Industrial Filters, Supply
of Spare Parts, Welding and Fabrications, Hydraulic Hose Assembly and repair, Maintenance
and service contracts.
Kampuni ya
Asfa Hose Service and Maintenance Support Ltd inapatikana maeneo ya Asilimia
Mia karibu na Front Oil Kahama. Mawasiliano yao ni 0715859321 au 0755067193 au
0767566233 au 0744446970 au Email : info@asfahoseservice.com
Website : www.asfahoseservice.com
na kwenye mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Instagram, Youtube @asfahoseservice
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...