WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amehimiza Wasanii nchini kuhakikisha wanamiliki Bima za Afya ambazo zitawasaidia wanapokua wagonjwa wakati wowote
Mhe. Bashungwa amesema hayo alipomtembelea Msanii Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini Kikumbi M. Mpango maarufu King Kikii Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2021.
"Wizara itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yako na kwasababu daktari wako tuna mawasiliano ya karibu tutakuwa tunajua hali yako inavyoendelea kila siku" amesisitiza Mhe. Bashungwa.
Kwa upande wake Msanii King Kikii amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kumtembelea na kumfariji pia amemuomba Waziri amfikishie Salam zake kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuliongoza Taifa.
Mzee King Kikii ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanamziki na wasanii wengine kuwa na nidhamu katika kazi ili kuendelea kufanya sanaa kwa muda mrefu.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...