Jafo ametoa msisitizo huo alipotembelea eneo la dampo kuu lilalotumika kuhifadhi taka ngumu.
Katika ziara hiyo Waziri Jafo ametoa wiki mbili kwa uongozi wa Jiji hilo kuhakikisha hali ya taka zilizosambaa hovyo katika dampo hilo kukusanywa vizuri kinyume na hali ilivyo sasa ambapo uchafu umeoneka kusambaa hovyo katika dampo hilo.
Meneja Msimamizi wa dampo hilo Bw. Marko Chacha amejitetea kwamba hali hiyo imetokana na kushindwa kufanyakazi ipasavyo kwa mitambo ya kushindilia taka kutokana na mvua.
Hata hivyo Jafo hakuridhishwa na utetezi wa Afisa huyo kwani Manispaa ya Moshi ambao wapo jirani kabisa na Jiji la Arusha wameweza kusimamia vyema dampo lao na kuwezesha uchafu wote kudhibitiwa vyema ndani ya dampo. Kutokana na hali hiyo Jafo ametoa wiki mbili ili hali hiyo irekebishwe ipasavyo.
Katika hatua nyingine Jafo amefanya ziara eneo la machimbo ya kifusi ya Isongo ambapo siku za hivi karibuni kulitokea maafa ya watu watatu kufariki na wengine kujeruhiwa kutokana na kudondokewa na kifusi cha udongo.
Katika eneo hilo
Waziri Jafo amemuagiza Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini Bw. Lewis Nzali
kukutana na Afisa anayesimamia sekta ya Madini wa Kanda hiyo ili waone namna
bora ya uchimbaji wa madini kwa kuzingatiwa suala la utunzaji wa mazingira.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...