Charles James, Michuzi TV
KATIKA kukabiliana na changamoto za uharibifu wa mazingira nchini na kuhakikisha utunzaji wa mazingira unakuepo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Selemani Jafo ameanzisha kampeni ya kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira huku akiwateua watu maarufu akiwemo Msanii Diamond, Mbunge Mariam Ditopile na wandishi Sakina Abdulmasoud, Oliver Nyeriga na Abubakary Famau kuwa mabalozi.
Katika orodha hiyo ya Mabalozi wa Kampeni hiyo wapo pia wasanii Shilole, nguli wa habari nchini Charles Hillary na wengine maarufu ambao kwa pamoja wanaunda Timu ya Mabalozi 40 watakaosaidia kampeni hiyo.
Akizungumza jijini Dodoma leo, Waziri Jafo Amesema kampeni hiyo inaenda sambamba na maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani ambayo itafanyika Juni 5 mwaka huu ambapo kampeni hiyo pia itazinduliwa.
Waziri Jafo amesema kupitia kampeni hiyo wanaamini itakua ni Suluhu ya kuhakikisha hali ya utunzaji wa mazingira inarejea nchini na itakua kampeni ya Nchi nzima huku ikienda sambamba na kauli mbiu ya 'Mazingira yangu, Tanzania yangu, naipenda daima' ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dk Philip Mpango.
" Kampeni hii inaenda Nchi nzima, tutahusisha kila idara zikiwemo Taasisi mbalimbali, Mikoa na Wilaya zake, Kata, Mitaa na Vijiji, Migodi na Viwanda na maeneo tofauti wakiwemo wadau wa usafi na mazingira na itaenda sambamba na utoaji tuzo kwa washindi katika kila kipengele," Amesema Waziri Jafo.
Baadhi ya mabalozi waliotwaliwa ni pamoja na Mhamasishaji wa Klabu ya Soka ya Yanga,Antonio Nugaz,muimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho,Mbunge wa Viti Maalum, Ester Matiko na mchekeshaji, Masanja Mkandamizaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Selemani Jafo akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo wakati akitangaza mabalozi 40 wa mazingira nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...