Mama Baraka ambae amewaomba Watanzania Kumsaidia kwa Hali na Mali ili aweze Kumlea Mtoto huyo mwenye Tatizo la Usonji.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Usonji (Lukiza Autism ) Hilda Nkabe akiwa pamoja na Balozi wa Taasisi hiyo Rose Manfere wakipokea Majukumu ya Mama Baraka ambae anapitia changamoto ya Maisha kutokana na Mtoto wake kuwa na Matatizo ya kitabia  pamoja na  Hali ya Usonji.

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
WADAU pamoja na Wazazi Watakiwa Kuishi vizuri na Watoto wenye Matatizo ya Usonji. Akizungumza na Michuzi Tv, Mwanzilishi wa Taasisi ya Lukiza, Autism Hilda Nkabe amesema Wadau mbalimbali wameonyesha Nia ya dhati Kusaidia watoto wenye usonji na kuwapa nafasi kushiriki nao vitu mbalimbali.

"Kwa upande wa Mbunge wa Kinondoni Abas Tarimba ameonyesha Nia yake na hata bungeni amekua akilikumbuka kundi la watoto hasa wenye Usonji pamoja na watoto wenye uhitaji."

Hata hivyo Nkabe amewaomba Watanzania Kumsaidia Mama wa Mtoto mwenye changamoto ya usonji (Mama Baraka) kutokana na kupitia kwake Maisha magumu.

"Nikiwa Kama mzazi wa Mtoto mwenye Usonji nakiri kusema Hali zetu Mara nyingi hazifanani lakini Mtoto Baraka mwenye umri wa miaka 13 amenigusa Sana na ningependa kuhamasisha wenzangu kujumuika Kumsaidia Mama huyu kwa kile kidogo watakachoguswa".

Mama Baraka ameeleza kwa namna gani changamoto anayoipata kwenye malezi ya Mtoto huyo B ambae alianguka akiwa na umri wa miaka 7 Shuleni na kupelekea kupata tatizo kwenye ubongo .

"Nimejaribu kufanya kazi nyingi lakini imekua ngumu kutokana na mtoto wangu kuharibu vitu vyangu pamoja na vya wafanyabiashara wenzangu imepelekea Hadi kunigombanisha na watu wa karibu yangu."

Mama Baraka amewaomba Watanzania Kumsaidia kwa Hali na mali ili aweze Kumlea Mtoto huyo kwani kwa Sasa mtoto huyo amekua na matatizo ya kitabia na kupelekea mama huyo kukosa muda wa Kuzalisha kipato ,pia ameshukuru timu nzima ya Lukiza Autism kwa kukubali Kushirikiana nae katika Malezi ya Mtoto wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...