Mkurugenzi wa Kampuni ya FPI Furaha Dominick akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Shindano la Kucheza lenye lengo la Kunyanyua vipaji kwa vijana.
Msanii Nurdin Bilal maarufu Kama Sheta akitoa neno kwa vijana wenye ndoto ya kutimiza vipaji vyao kwa kupitia Sanaa.


  Na Khadija Seif, Michuzi Tv

WASHINDI watakaopatikana katika Shindano la kucheza (Dance) watapata fursa ya Kutengenezewa mazingira mazuri ya ajira ya kudumu kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kujiepusha na mazingira ya vitendo viovu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam  Mkurugenzi wa Kampuni iliyoandaa Shindano la kucheza (FPl) Furaha Dominick amesema Mashindano ya kudansi yaliyopewa jina la (FDT) ni kwa lengo la kusaidia vijana wenye vipaji hivyo.

"Lengo ni kusaidia vijana pamoja na kuvumbua vipaji vilivojificha, hivyo kuwepo kwa shindano kamahili  itasiaidia mno kujua vipaji hasa vya kucheza." Amesema.

Hata hivyo Dominick amesema wanatarajia kuanza rasmi shindano hilo mapema Juni 5 mwaka huu huku vigezo na masharti vikifafanuliwa zaidi.

"Shindano litaanza rasmi Dar es salaam Juni 5  katika viwanja vya Donbosco Oysterbay na wanaoweza kushiriki ni kuanzia Miaka 18."

Imeelezwa pia, Mshindi pia  atapata fursa kushiriki shindano la Kimataifa 

Kwa upande wake Msanii wa Bongofleva Nurdin Bilal maarufu kwa jina la "Shetta" amewaomba vijana kukimbilia fursa hiyo ili kuweza kutimiza malengo yao.

"Kabla sijaanza Kuimba nimepitia mikono ya msanii mkongwe Dully sykse nimecheza nyimbo zake yaani Mtumbuizaji kwa miaka mingi ndipo nikahamia Kwenye Muziki hivyo utaona nafasi ama fursa moja ilivoweza kuanzisha nyingine ." Amesema.

Hata hivyo Shetta amesema jinsi ya kushiriki shindano hilo ni kufika ofisi za Furaha tv Mikocheni Dar es salaam na fomu zitatolewa  bure kabisa.

Shetta ametaja Zawadi kwa Mshindi wa Kwanza ni fedha taslim Milioni 10,wapili milioni 5, huku wa Mwisho akipatiwa Laki 5.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...