MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla leo Mei 26 amefanya kikao kazi na watendaji wa Taasisi Mbalimbali zilizopo Dar es salaam ikiwemo DAWASA, TRA, TANESCO, TANROAD, TARURA na DMDP ambapo ametaka kila Taasisi kutekeleza wajibu wake ili kuondoa kero kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, RC Makalla amewapongeza TRA kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa Mapato kwa Mwezi huu na kuwaelekeza kuendelea kukusanya mapato kwa mujibu wa sheria pasipo kuwabugudhi wananchi huku akisisitiza utoaji wa elimu kwa walipa Kodi.

Aidha RC Makalla amewataka TANROAD na TARURA kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye Barabara zao na kufanyia ukarabati sehemu zenye changamoto ili kuondokana na kero ya ubovu wa Barabara.

Aidha amewataka kusimamia ipasavyo miradi ya barabara huku akielekeza DMDP kushirikiana na Halmashauri kuweka moundombinu bora ya kuhakikisha masoko yote yaliyojengwa yanaanza kutumika baada ya kubaini masoko mengi yaliyojengwa yamekosa wapangaji.

Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TANESCO kuhakikisha inafanyia kazi changamoto ndogondogo zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mapema kwa wananchi pindi inapotokea matengenezo au hitilafu ili watu wajiandae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...