*******************************
Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu kama Fred Vunjabei jana tarehe 23 May 2021 amepitishwa na Baraza kuu la UVCCM kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha kupitia kikao cha Baraza Kuu ambacho kimemalizika jana Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Kamati ya utekelezaji chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Kheri James ilikuja na pendekezo la jina la mwenyekiti huyo wa kamati ambapo baadae alithibitishwa na wajumbe kwa kura nyingi za ndio huku katibu wake akifahamika kwa jina la Rose Manumba, Baraza lilichagua wajumbe wengine wanne wa kamati kutoka bara na visiwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...