Meneja wa Kiwanda cha Kairuki Pharmaceuticals Industries Limited (KPIL), Hellen Majita akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alipotembelea kiwanda hicho Zegereni Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki na kuwahakikishia umeme wa uhakika.
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akizungumza na Mkurugenzi wa Hospitali ya Kairuki, Dk. Muganyizi Kairuki (kushoto) alipotembelea kiwanda cha Kairuki Pharmaceuticals Industries Limited (KPIL) Zegereni Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki na kuwahakikishia umeme wa uhakika .
Meneja wa Kiwanda cha Kairuki Pharmaceuticals Industries Limited (KPIL), Hellen Majita akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alipotembelea kiwanda hicho Zegereni Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki na kuwahakikishia umeme wa uhakika.

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nishati, Medard Kalemani amewahakikishia wenye viwanda eneo la Zegereni Mkoa wa Pwani kuwa serikali itawapatia umeme wa uhakika hivyo kuwawezesha kuzalisha bidhaa bila shida ya umeme.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea kiwanda cha Kairuki Pharmaceuticals  Industries Limited (KPIL), kilichoko eneo la viwanda Zegereni mkoani Pwani, kukagua mradi wa kufikisha umeme eneo hilo.

Waziri Kalemani amesema pamoja na mradi huo wa umeme serikali pia inatekeleza mradi wa kuwafikishia gesi asilia ili viwanda vitumie umeme pamoja na gesi katika shughuli zao za kila siku.

"Serikali imeshakamilisha mradi wa kukiongezeda uwezo kituo cha kupoza umeme cha Mlandizi ambacho awali kilikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha umeme na sasa umeongezeka kutoka Megawati 40 hadi Megawati 96 huku mahitaji ya mkoa huo ni Megawati 55 hivyo Mkoa huo utakuwa na ziada ya Megawati 40.

Naye, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kairuki, Dk. Muganyizi Kairuki, amesema maandalizi yote yamekamilika kwaajili ya kiwanda kuanza kuzalisha.

 Dk. Kairuki amesema hata malighafi za kutengeneza dawa zimeshaagizwa kutoka nje ya nchi na zinatarajiwa kufika mwezi Mei na wafanyakazi wa kiwanda hicho wameshapatikana.

Aidha, alisema jumla ya uwekezaji huo uliopo eneo la viwanda Zegeleni Manispaa ya Kibaha ni Sh bilioni 45 ambazo ni mkopo.

 Amesema asilimia 60 ya dawa zitakazokuwa zinatengenezwa zitakuwa zikiuzwa kwenye soko la ndani wakati asilimia 40 zitauzwa kwenye soko la nchi za Afrika Mashariki (EAC) nan chi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Ameongeza kuwa, kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha chupa za dawa 55,000,000 kwa mwaka na kutengeneza ajira za moja kwa moja 200 na ajira za muda zipatazo 500.

Amesema watazalisha dawa za aina mbalimbali nchini kwa kutumia teknojia ya kisasa zaidi hivyo kupunguza utegemezi wa kununua dawa hizo nchi za nje hivyo kuokoa fedha nyingi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni alitembelea kiwanda hicho ambapo alisifu uwekezaji uliofanywa na Kairuki na kuahidi kuwa serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...