TAASISI ya FURAHIKA Education College imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi laki 6 ikijumuisha jezi, mipira na trucksuit huku lengo kuu ikiwa ni ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali hasa kwa kutoa elimu bure na kuboresha sekta ya michezo mashuleni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ilala jijini Dar es Salaam mratibu wa miradi ya michezo kwa watoto mashuleni kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Furahika Education College, David Msuya amesema, katika maandalizi ya michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA taasisi hiyo imetoa jezi, mipira na tracksuit kwa ajili ya maafisa wa michezo kwa wilaya za Kigamboni, Ubungo na jiji la Ilala ili ziweze kushiriki na kushinda katika mashindano hayo.
Msuya amesema, taasisi hiyo imekua ikishiriki katika uboreshaji wa elimu pamoja michezo mashuleni katika kuwajenga wanafunzi na amewashauri wadau wengine kuunga mkono jitihada hizo kwa kutoa vifaa na kushiriki kukarabati maeneo ya michezo vikiwemo viwanja.
Kwa upande wake mratibu wa michezo Mkoa wa Dar es Salaam Adolf Ally amesema, vifaa hivyo vitaleta tija mashuleni na kuwaomba wadau wengine kuisaidia Serikali inayotoa elimu burekwa kuisaidia sekta ya michezo mashuleni kwa kutatua changamoto ya viwanja vya michezo na na vifaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...