Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
KITUO
cha Msaada wa kisheria Kibaha Paralegal Center (KPC) kinatarajia kutoa
elimu ya kisheria kwa watu zaidi ya 40,000 katika mji wa Kibaha kwa
mwaka huu ,ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo viongozi wa serikali za
mitaa,hali itakayowasaidia kubaini haki zao za msingi .
Hatua
hii inakwenda kuwapa ufahamu wananchi juu ya masuala mbalimbali ya
kisheria hivyo kupunguza changamoto za vitendo vya kuvunja sheria hasa
migogoro ya ardhi,ukatili wa kijinsia ambapo kwa kipindi cha nyuma watu
wengine walikuwa hawajui sheria zinazopigania haki zao .
Katibu
wa kituo hicho Dismas Chihwalo alieleza,lengo la kuwajengea uwezo
viongozi hao juu ya masuala ya sheria ni ili waje kuwasaidia wananchi na
kuwaelekeza njia za kufuata ili wapate haki zao.
Chihwalo
alibainisha , viongozi hao ndiyo watu wa mwanzo kupata taarifa juu ya
masuala mbalimbali yanayokwenda kinyume cha sheria kutoka kwa wananchi
wanaowaongoza na kituo kinatoa msaada wa kisheria bure kwa watu kwenye
uhitaji wakiwemo wanawake.
“Mbali
ya kuwajengea uwezo viongozi juu ya masuala ya kisheria," tunatoa elimu
ya sheria na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ili kutatua migogoro
ya kisheria kabla ya kufika kwenye vyombo vya kisheria ili kuvipunguzia
mzigo vyombo vya kisheria,”alisema Mlenga.
Alisema
,baada ya kuwajengea uwezo viongozi wa kata na mitaa wanatoa elimu na
msaada wa kisheria kwa wananchi, wanafunzi wa shule ya Sekondari
Mwanalugali na shule ya Msingi Tumbi juu ya sheria ya mtoto na makundi
ya vikoba kwenye kata ya Tumbi.
"Kutokana
na elimu na msaada wa kisheria tunaotoa kwa wananchi wa Halmashauri ya
Mji wa Kibaha mabadiliko yameanza kutokea ambapo wananchi wamenza kuwa
na uelewa juu ya kutoa taarifa za vitendo vya ukiukaji wa sheria,"
alisema Chihwalo.
Nae
mwenyekiti wa mtaa wa Mwanalugali Deo Rwekaza alisema kuwa mafunzo hayo
yanawasaidia ili wananchi wanapofika ofisini kwake wanapokuwa na
migogoro wanawaelekeza njia nzuri ya kuwasaidia kutatua changamoto za
baadhi ya migogoro.
Rwekaza
alieleza, baadhi ya wananchi wanapokuwa na migogoro wanakuwa hawajui
nini cha kufanya au hatua za kufuata mara changamoto ya migogoro
inapotokea kabla ya kwenda kwenye vyombo vya kisheria ambako serikali
inajitahidi kuhakikisha watu wanaishi kwa Amani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...