Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi Amandus Chinguile amekabidhi mifuko ya saruji 1,800,Mei 22 /2021 ikiwa ni Moja ya  ahadi yake katika sekta ya  ELIMU  aliyoitoa wakati akiomba ridhaa katika uchaguzi Mkuu 2020.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika kata 16  kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule za sekondari ndani ya kata hizo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Amandus Chinguile alisema 'yeye kama Mbunge anao wajibu wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki kwa kuwaboreshea miundombinu.

Alisema kuwa ataendelea kuziangazia shule zenye changamoto na kuziwekea mazingira rafiki ya kujifunzia.

Vifaa hivyo vinatarajia kutumika kakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa  22 katika Shule za Sekondari zilizopo Jimboni humo.

"Ni wajibu wetu sisi kama viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja   kuinua Elimu katika wilaya yetu kwa kuhakikisha tunaiboresha Miundombinu ya shule"Alisema Chinguile.

Aliongeza kuwa, hii awamu ya kwanza  ameziangazia kata 16 katika sekta ya Elimu,akini ataendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika kata nyingine.

'Ili Jimbo  liendelee kupiga hatua kimaendeleo nitaendelea kutatua kero zinazowakabili wananchi  kwa kuimarisha miradi ya Maendeleo katika sekta ya Maji,Afya ikiwemo kuisimamia Serikali katika sekta ya Kulimo ili pembejeo za Kilimo ziweze kuwafikia kwa wakati na zipatikane kwa bei nafuu.

Akiangazia sekta ya Elimu alisema,bado hitaji ni kubwa hivyo ni jukumu la kila mdau kuendelea kuchangia ili changamoto zinazoikabili sekta hiyo ziweze kumalizika na wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki ili kuongeza ufahuru.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...