Watu wapatao 11 wanaripotiwa kufa baada ya mlipuko wa volcano katika Mlima Nyiragongo, Mashariki mwa Congo DRC na kiasi cha kilomita 10 kutoka mji wa Goma ulio na wakazi takriban milioni mbili.
Msemaji wa serikali Patrick Muyaya ameviambia vyombo vya Habari kwamba mamia ya Watoto hawajulikani walipo hadi hivi sasa kwa kupotea ama kupotezana na familia zao baada ya mlipuko huo kutokea Jumamosi jioni.
Muyaya kasema watu watano walipoteza Maisha wakati wakijaribu kuondoka eneo la mlipuko, wakati wafungwa wanne walikufa wakati wakijaribu kutoroka kutoka katika gereza la Munzenze.
Watu wengine wawili wameripotiwa kupoteza maisha siku ya Jumapili.
Mlipuko huo, uliosababisha zaidi ya raia wa DRC 8,000 kukimbilia nchini Rwanda, hivi sasa unaripotiwa kutuama baada ya kuangamiza makazi 600 ya mji wa Goma Pamoja na shule tano.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...