KUELEKEA mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISETA kwa shuke za Sekondari mkoani Dar es Salaam mratibu wa michezo kwa watoto mashuleni katika ngazi ya Wilaya na Mkoa, David Msuya ameendelea kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa Wilaya mbalimbali ili kuwawezesha wanafunzi hao kushiriki vyema na kushinda katika michezo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam Msuya amesema, kupitia Taasisi ya Furahika Education College wamekabidhi mipira kwa shule za Wilaya za Ubungo, Temeke, Ilala na Kigamboni ili kuiunga mkono Serikali katika juhudi za kujenga taifa la vijana imara.

Amesema Taasisi hiyo haitoacha kusaidia masuala ya uboreshaji elimu na suala zima la michezo mashuleni na kuwataka wadau wengine kujitokeza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya michezo  ikiwemo ubovu  wa viwanja michezo na uhaba wa vifaa vya michezo.

Mapema wiki jana Msuya kupitia Taasisi ya Furahika Education College alikabidhi  mipira, jezi na tracksuit kwa maafisa wa michezo ikiwa ni mchango wao kwa sekta ya michezo kwa watoto mashuleni pamoja na kuisaidia serikali ambayo imekuwa ikihakikisha watoto wanapata elimu bure bila malipo.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...