Na Amiri Kilagalila,NJOMBE
Naibu
waziri wa nchi,ofisi ya Rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa
(TAMISEMI) ambaye ni mbunge wa jimbo la Wanging'ombe mkoani Njombe
Dkt,Festo Dugange amesema licha ya kuwa kata ya Uhenga inaongozwa na
diwani wa Chama cha upinzani (CHADEMA), bado ataendelea kuhakikisha
shughuli za kimaendeleo zinaendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika kijiji hicho cha
uhenga mbuge huyo Dkt,Dugange amewahakikishia wananchi kuwa atatekeleza
miradi mbalimbali ya kimaendeleo bila upendeleo.
Aidha
Dkt Dugange amesema kuwa ataendelea kushirikiana na diwani aliyepo kwa
sasa madalakani kwa sasa kwa kuwa lengo lao kwa sasa ni kuwahudumia
wananchi kwa kuwapelekea maendeleo.
Awali
akizungumza katibu wa umoja wa wanawake wilayani Wanging'ombe (UWT)
Fatma Ngole amewataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaodai kuwa
Uhenga haitatekelezewa miradi ya kimaendeleo kwa kuwa imechagua kiongozi
kutoka chama cha upizani cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Kwa
upande wake diwani wa kata hiyo ya Halfan Kawambwa amewashukuru
viongozi wa wilaya hiyo kwa ushirikiano wanaotoa kwake na kueleza kuwa
kwa sasa hakuna haja ya kuendeleza mambo ya kisiasa kwa kuwa uchaguzi
umeshapita.
Kata ya Uhenga ni kata pekee kati ya kata 21 inayoongozwa na upinzani huku kata zingine zikiongozwa na Chama cha Mapinduzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...