Mkurugenzi wa Udhibiti, Ufuatialiaji na Tathimini wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE, Dk Geofrey Okele akizungumza na Wandishi wa Habari jijini Dodoma leo wakati akitangaza kuzinduliwa kwa dirisha la udahili kwa wanafunzi wa ngazi ya astashahada na stashahada nchini.

Charles James, Michuzi TV

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi NACTE limetangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili wa wanafunzi katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa kozi zote zinazotolewa na Vyuo vya Elimu ya Ufundi .

Akizungumza na Wandishi wa Habari jijini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Udhibiti, Ufuatiliaji na Tathmini wa NACTE, Dkt. Geofrey Okele, ameeleza kuwa dirisha hilo la udahili limefunguliwa rasmi Mei 27 mwaka huu hadi Agosti 14 mwaka huu katika awamu ya kwanza .

Amesema kuwa kufuatia kufunguliwa huko kwa dirisha hilo Vyuo vinaruhusiwa kupokea maombi ya udahili kuanzia leo Mei 27 hadi Agosti 14 na Vyuo vinapaswa kuchagua waombaji walio na sifa kuanzia Agosti 21 hadi Septemba 3 mwaka huu na majina ya waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki.

Dk Okele amesema majina ya waliochaguliwa na NACTE yatatangazwa na Vyuo husika Septemba 16 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kwa mwaka wa masomo Novemba Moja mwaka huu.

" Aidha waombaji wa Kozi za Afya kwenye vyuo vya serikali watatuma maombi yao moja kwa moja kupitia tovuti ya NACTE kuanzia leo Mei 27 hadi Agosti 14 mwaka huu na majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa Agosti 22 mwaka huu.

Vyuo vyote vya elimu na mafunzo ya ufundi vitakavyopokea maombi ya wanafunzi kwa ngazi ya astashahada na stashahada vinaelekezwa kuzingatia taratibu za udahili kama zilivyotolewa na Baraza kwa mwaka wa masomo 2021/22," Amesema Dk Okele.

Amesema wahitimu wote wa Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za astashahada na stashahada wanashauriwa kufanya maombi hayo kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi wanazozipenda na walizotimiza sifa za kujiunga nazo kwa mwaka huu mpya wa masomo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...