Mkutano mkuu Umoja wa mafundi cherehani wa mkoa wa Dodoma (UMACHEDO) umefanyika leo katika hoteli ya Dodoma kwa mafanikio makubwa huku ukihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Dr.Hashil Abdallah(kwa niaba ya Mh. Waziri Prof. Kitila Mkumbo),Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Anthony Mtaka na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Viwanda na Biashara,Naibu Katibu Mkuu Dr. Hashil Abdallah amewapongeza mafundi cherehani wa Dodoma kwa kuja na wazo la kuunda umoja wao na kutumia fursa hiyo kuwaahidi mafundi hao kupata mikopo kupitia mfuko wa wajasiriamali (NEDF),uwezeshwaji wa vyerehani kwa mikopo nafuu na semina mbalimbali za mafunzo kupitia SIDO.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.Anthony Mtaka amewapongeza UMACHEDO kwa kuungana pamoja na kuwataka kuchangamkia fursa zilizopo Dodoma badala ya kuwa waangaliaji wa fursa zilizopo Dodoma na kuwahakikishia ushirikiano kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuwawekea mazingira rafiki katika utoaji wa huduma zao katika shughuli mbalimbali za kiserikali zikiwemo mbio za Mwenge.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ambaye pia ni Mlezi wa UMACHEDO ameahidi kuwaunganisha mafundi hao na Taasisi za NSSF,SIDO na NHIF kwa lengo la kuwanufaisha zaidi wananchama na kuahidi kusimamia kwa karibu upatikanaji wa mashine za kisasa za kushonea kupitia mkopo utokanao na Mfuko wa Taifa wa Wajasiriamali** (NEDF)** na Benki ya Azania.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Hashil Abdallah.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Anthony Mtaka

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Hashil Abdallaha akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Anthony Mtaka na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Anthony Mtaka akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Anthony Mtaka na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...